Tuesday, February 25, 2014

NA:MWAJUMA ABDUL

 Wanafunzi wa kike wanavyoangukia kwenye mikono ya wanaume wakware

 
Picha hizi zinatoa ushuhuda wa vikwazo wanavyokumbana navyo wanafunzi wa kike wakiwa njiani kwenda au kurudi shule.
Mwandishi wetu alimwona mwanafunzi huyu akizongwa na kijana huyu mkware katika eneo la makaburi ya Bahi Road mkoani Dodoma.
Japo wahusika walionekana kujuana, msichana huyu anayesoma Shule ya Sekondari Kikuyu iliyopo Manispaa ya Dodoma, alikiri kuwa maongezi yao yalikuwa yakielekea kubaya kiasi cha kuamua kukimbia.
Kadhia hii ilimkumba msichana huyu akiwa njiani. Anapoishi na ilipo shule kuna umbali wa karibu kilomita tano.

Vikwazo kwa watoto wa kike
Pamoja na mikakati iliyopo ya kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu, hali halisi katika maeneo mengi nchini inaonyesha kuwa bado kuna vikwazo mbalimbali vinavyowazuia wasichana kupata haki hiyo ya msingi
.
Kwa mfano, mara kwa mara wadau wa elimu kupitia ripoti zao wamekuwa wakisema watoto wa kike nchini wakiwamo wanafunzi hawako salama.
Wanafunzi hao ni waathirika wakubwa wa vitendo mbalimbali vya unyanyasaji wa kijinsia ikiwamo kubakwa. Ukweli ni kwamba wanafunzi wa kike hawako salama nyumbani, njiani wanapoelekea au kurudi shule na hata shuleni kwenyewe.
CHANZO:MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment