Tuesday, February 25, 2014

Rais Obama ameagiza makao makuu ya ulinzi nchini Marekani Pentagon kuandaa mipango ya kuwaondoa wanajeshi wote kutoka Afghanistan ifikapo mwisho wa mwaka huu iwapo hakutakuwepo maafikiano rasmi na Serikali ya Afghanistan.



Wapiganaji wa Taliba

Rais Obama alimpigia simu Rais Karzai wa Afghansitan juu ya mpango huo na Rais Karzani amwaudhi Marekan kwa kukataa kutia sahihi muafaka ambao ungeruhusu baadhi ya wanajeshi kuendelea
kukaa Afghanistan baada ya muda uliokubaliwa awali wa mwisho wa mwaka huu wa 2014 .
Mpango huo ambao  ulikuwa umekubaliwa na baadhi ya viongozi wa kikabila la Afghanistan - unaandaa wajibu wa wanajeshi wa NATO unaoshirikisha kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Afghanistan na kusaidia Serikali ya taifa hilo kukabiliana na wapiganaji wa Kitaliban.
Mkataba huo pia unawapa kinga ya kisheria wanajeshi wa Marekani walioko nchini Afghanistan.
Ikulu ya White House imesema kuwa hakuna uwezekano wa Karzai kutia sahihi mapatano hayo kabla ya kuondoka mamlakani Aprili mwaka huu.kutoka BBC swahili

0 comments:

Post a Comment