Tuesday, October 7, 2014

UJASIRIAMALI NI MKOMBOZI WA MAISHA..ARUSHA

Mkurugenzi wa mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha bwana Joseph Mayagila Akifungua semina ya ujasiriamali iliyofanyika chuoni hapo hivi karibuni...
habbari na Yasinta Peter
Wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wametakiwa kujishughulisha na biashara pamoja na kuwa na tabia ya kujiwekea akiba kwa ajili ya maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa chuo hicho Bw.Joseph Mayagila  wakati akifungua semina ya ujasiriamali ambayo ilifanyika kwa siku tatu chuoni hapo kuanzia tarehe 1 mpaka tarehe 3 Octoba mwaka huu chuoni hapo.

Bw.Mayagila ameongeza kuwa wanafunzi wengi hawana tabia ya kujiwekea akiba katika fedha ambazo wanatumiwa na wazazi wao kwa ajili ya matumizi na kuwaasa wanafunzi hao wawe wanajiwekea akiba kwa maendeleo yao.

Katika semina hiyo walimu wa chuo hicho waliyoa mada mbalimbali zikiwemo za mpango wa biashara,miongozo ya mjasiriamali,namna ya kutathmini biashara pamoja na nyingine nyingi ambapo wanafunzi wote wa chuo hicho walishiriki.

Pia ili kuongeza vionjo katika semina hiyo kulikuwepo na  burudani mbalimbali ambapo wanafunzi walipewa fursa ya kuonyesha vipaji vyao mbele wanafunzi wenzao na burudani hizo ni pamoja na kuimba pamoja na vichekesho.

Nao wanafunzi wa chuo hicho wamesema kuwa wamefurahishwa na uwepo wa semina hiyo kwa sababu imewafunza mambo mbalimbali juu ya ujasiriamali ambayo hawakuwa wakiyafahamu.

Mmoja wa wanafunzi hao Bi.Edna Lucas alikuwa na haya ya kusema,
‘’Semina ni nzuri na nimeweza kujifunza mambo mengi ambayo sikuwa nayajua na kwa kupitia semina hii nimehamasika kufanya biashara’’.

Akizungumza ili kuhitimisha semina hiyo makamu mkuu wa chuo Bw.Elifuraha Samboto amewataka wanafunzi  kuwaheshimu walimu na vilevile wawe na tabia ya kjisomea.

Bw.Samboto alimaliza kwabkuwashukuru walimu na wanafunzi kwa ushiriki wao katika semina ya jasiriamali.

0 comments:

Post a Comment