Friday, February 14, 2014

Kenya:'Marekani inachochea mapinduzi'




Mwanamke akibeba msaada kutoka USAID
Serikali ya Marekani imekanusha madai ya serikali ya Kenya ya kuwafadhili wanaharakati kuchochea mapinduzi nchini Kenya.
Balozi wa Marekani Robert Godec alikanusha
madai hayo akisema miradi yao yote nchini Kenya imeruhusiwa na serikali.
Godec alisema serikali yake imekuwa ikichangia maendeleo na utawala bora nchini Kenya kwa kipindi cha miaka 50.
Kamati ya kitaifa ya maswala ya Usalama nchini Kenya NSAC ,imeilaumu shirika la misaada la Marekani USAID kwa kufadhili mashirika yasio ya kiserikali yanayopinga serikali ya Rais Uhuru Kenyatta.
Katika barua hiyo mwenyeketi wa kamati ya usalama Francis Kimemia alidai kuwa serikali ina habari za kijasusi zinazodhibitisha kuwa USAID imekuwa ikitoa maelfu ya dola kwa wanaharakati Boniface Mwangi na John G, kufanikisha maandamano mjini Nairobi.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji jijini Nairobi.
Waandamanaji hao walikuwa wanalalamikia kutelekezwa kwa mamilioni ya wakenya na utepetevu wa utawala uliopo.
"Maandamano haya yalikuwa ya amani kupinga utepetevu wa serikali yetu. Visa vya ubadhirifu wa pesa za uma vimeenea kote. Usalama umezorota na vijana hawana kazi, lakini hii serikali haitaki kuelezwa ukweli."
Boniface Mwangi
Mratibu wa maandamano hayo Boniface Mwangi alipinga madai hayo.. Mwanaharakati mwingine mashuhuri nchini Kenya Timothy Njoya aliyeshiriki katika maandamano ya hapo jana, amesema kuwa madai ya serikali ya Kenya ni ya kipuuzi.
husiano baina ya Kenya na Marekani ulidhoofika mwaka uliopita, baada ya aliyekuwa Ubalozi wa Marekani kuonya wakenya kutowapigia kura watuhumiwa wa kesi za mauaji ya halaiki Uhuru Kenyatta na William Ruto.
Madai hayo yalitiliwa pondo juma lililopita na ripoti iliyomnukuu aliyekuwa kiongozi wa mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini Hague Uholanzi, Louis Moreno Ocampo akikiri kuwa alishinikizwa na mataifa ya magharibi kuweka vikwazo ili kuwazuia wawili hao wasiwanie urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Machi mwaka uliopita.
Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto wamezilaumu mataifa za kigeni kwa kesi dhidi yao katika mahakama ya ICC.

0 comments:

Post a Comment