Saturday, February 15, 2014

Serikali yakiri kuwapo kwa sukari ya kutosha nchini


Serikali imesema taifa lina sukari ya kutosha na kuwaondolea wananchi hofu ya kutokea uhaba wa bidhaa hiyo mwaka huu.

Akizungumza na chombo hiki Jumamosi, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari , Henry Semwaza
, alisema uzalishaji wa sukari umekuwa mkubwa ukilinganishwa na mahitaji.

“Mwaka huu wananchi wasihofie uhaba wa sukari, kwani uzalishaji umekuwa mkubwa na baadhi ya viwanda vimeanza kuzima mitambo yao baada ya msimu kumalizika,” alisema Semwaza na kutaja kampuni ya Mtibwa ya Morogoro kuwa imepumzisha mitambo yake.

“Viwanda vya Kilombero 1 na 2, Kagera na TPC Ltd, vipo mbioni kuzima mitambo yao, lakini vinatarajiwa kuanza tena kazi ifikapo Mei mwaka huu , hata hivyo kufunga uzalishaji kwa muda kusiwatie wananchi wasiwasi kwani sukari ipo ya kutosha,” alisema. Alieleza kuwa wastani wa uzalishaji wa sukari kwa mwaka ni tani 300,000 lakini mahitaji ni tani laki 5.9, na kwamba 200,000 zinatumiwa kwa uzalishaji viwandani.

Alisema serikali haitarajii kutoa vibali vya kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje kwa sababu inapatikana ya kutosha kwenye soko la ndani.

CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment