Tuesday, February 25, 2014

Haki ya matibabu Uganda Licha ya sheria








Waziri wa afya nchini Uganda, Daktari Ru-hakama Rugunda, amesema kuwa wapenzi wa jinsia moja hawatabaguliwa watakapokuwa wakihitaji huduma ya matibabu.

Mashirika ya kupambana na ukimwi yamesema sheria hiyo itakuwa na athari mbaya katika juhudi za kukabiliana na kuenea kwa virusi vya HIV.
Daktari Rugunda alisema kuwa wapenzi wa jinsia moja
wanapaswa kuwa wazi kwa watabibu, hasa wakati wanapojadiliana maswala ya virusi vinavyosababisha ukimwi, HIV.

Huduma duni ya afya nchini Uganda hutegemea zaidi misaada kutoka wafadhili wa kimataifa.
Hadi kufikia sasa Marekani imesema kuwa inachunguza upya misaada kwa mipango kadhaa inayogharamia nchini humo.
Daktari Rugunda amesema kuwa ana imani kuwa  Marekani haitapunguza misaada  ya kifedha lakini akasisitiza kuwa ikichukua hatua hiyo Uganda itaendelea na shughuli zake kama kawaida.kutoka BBC
Na mwandishi wako
Lightness urassa

0 comments:

Post a Comment