Monday, February 17, 2014

Kundi moja lenye mafungamano na al-Qaïda latekeleza shambulizi katika mji wa Sinaï nchini Misri


milipuko uliyoteketeza basi liliyokua likisafirisha watalii na kusababisha vifo
vya watu 3 na wengine 13 kujeruhiwa,mjini Taba,
*Kundi moja lenye mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaïda linashukiwa kutekeleza jana jumatatu katika mji wa Sinaï shambulio ambalo limelenga kundi la watalii kutoka Korea ya Kusini. Shambulio hilo limetokea katika eneo la Taba linalopatikana katika mji wa Sinaï. Kwa mujibu wa duru za kiusalama, watu watatu wameuawa, wakiwemo watalii wawili na dreva, ambaye ni raia wa Misri. Watu kumi na tatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo.
Naibu waziri wa mambo ya ndani, abdel Fattah Osman, amefahamisha kwamba uchunguzi umeanzishwa na imebainika kuwa basi liliyokua limewasafirisha watalii limelipuliwa na mtu ambaye amepenya karibu na mlango wa basi.
Utafiti wa vipimo vya damu umeanzishwa ili kujua iwapo kuna mtu wa nne ambaye ataweza kuwa amejilipua. Awali polisi ilifahamisha kwamba basi hilo lililipuliwa na bomu liliyotegwa kupitia simu ya mkononi. Hata hivyo shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa kupitia tovuti na kundi la waislamu wenye itikadi kali la Ansar Beit al-Maqdess.
Kundi hilo lenye mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaïda, limebaini kwamba lilikua limewapa watalii hao muda wa siku nne wawe wameondoka kwenye aridhi ya Misri. Ansar Beit al-Maqdess, lilianziasha rasmi harakati zake dhidi polisi na jeshi, baada ya kutimuliwa madarakani kwa aliekua rais Misri Mohamed Morsi. Kundi hilo lilikiri majuma mawili yaliyopita kuendesha shambulizi dhidi ya helikopa ya kijeshi ambayo iliteketea baada ya kupigwa roketi.
Mashambulizi dhidi ya watalii ni mbinu nyingine ambayo waislamu wenye itikadi kali wamekua wakitumia katika miaka ya 1990. Mashambulizi hayo yaliwalenga wanasiasa na wanajeshi, na baadae kanisa na waumini wa dini zenye madhehebu ya kikristo.
Na mashambulizi mengine yaliwalenga watalii, kama ilivyotokea jana jumapili. Wanamgambo wa kiislamu wamekua wakiwachukulia watalii kama ndio wanazagaza madhambi.

Inaelekea kua kundi la Ansar Beit al-Maqdess, kama makundi mengine ya wanamgambo wa kiislamu wenye itikadi kali katika miaka ya 90, wamekua wakichukulia kwamba mashambulizi dhidi ya watalii ni kupelekea sekta ya utalii ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Misri inaathirika, na hivo kusababisha utawala unakosa mapato kutoka sekta ya utalii.
nayo yakijiri, rais aliyeondolewa madarakani na jeshi nchini Misri Mohamed Morsi ameshutumu kuhusu kunyimwa uhuru wa kujieleza kwa kuwekwa kwenye kizimba kinachozuia sauti, wakati wa kuanza kusikilizwa kwa kesi yake kuhusu shutuma za upelelezi Jumapili Jana huku wanasheria wake wakisusia kuendelea na kesi hiyo.
Kesi hiyo ni ya tatu kwa kiongozi huyo wa kiislam tangu kupinduliwa kwake mwezi Julai 3 imeahirishwa leo Jumapili hadi februari 23 ili kuruhusu wanasheria kuchagua wanasheria wapya.

Morsi, ambaye alipaza sauti kuwa yeye ni rais halali na aliyechaguliwa kuwa rais wa Misri wakati wa kusikilizwa kwa kesi zingine dhidi yake ,amesema kuwa mahakama inajaribu kumnyamazisha.


0 comments:

Post a Comment