Friday, August 29, 2014

TANZANIA NA BURUNDI ZAIMARISHA ALAMA ZA MIPAKA YAKE.....

Shughuli ya kuweka alama mpya ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi inaendelea, ambapo nchi hizo mbili jirani zinapima na kuweka mawe ya kimataifa kati ya mipaka. 
 Hafla rasmi ya zoezi hilo ilizinduliwa jana upande wa Tanzania katika kijiji cha Mugikomelo mpakani mwa nchi hizo mbili na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa nchi mbili. Katika hafla hiyo Rais Pierre Nkurunziza  wa Burundi amewashukuru Watanzania wote kwa mchango wao mkubwa katika kueleta amani na utulivu katika nchi yake, akisisitiza kuwa, licha ya nchi mbili hizo kuwa na mpaka lakini Tanzania inaruhusu maelfu ya wakimbizi wa Burundi kuingia nchini kwake bila kufuata taratibu za mipaka na uhamiaji, kwa sababu ya matatizo yanayowakabili  Warundi.
 Uwekaji mawe kwenye mpaka wa kimataifa kati ya nchi hizo mbili, unafanyika ikiwa ni baada ya kukamilika mchakato mrefu uliohusisha wataalamu wa nchi hizo wa kupima theluthi moja tu ya mpaka huo wa nchi mbili wenye kilometa 451.
Mpaka wa Tanzania na Burundi ni wa tano kwa urefu kati ya nchi 8 jirani na Tanzania, huku  Kenya ikiwa na mpaka mrefu zaidi wenye kilometa 769.


CHANZO: BBC
HABARI NA STEVEN  MULAKI

0 comments:

Post a Comment