Tuesday, February 25, 2014

TATIZO LA UNYESHAJI MVUA KATIKA SOKO LA KWA MOROMBO JIJINI ARUSHA.

 Na mwandishi wako Vivian E. Japhet.

Baadhi ya biashara za sokoni hapo.


Wafanyabiashara wa soko  la kwa Morombo  lililopo jijini Arusha  wameitaka serikali iwajengee soko la   kudumu ili waepuke usumbufu kutoka kwa manispaa.
Bidhaa za  sokoni hapo  zinazouzwa kwa bei ya jumla.
Akiongea na waandishi wa
habari mmoja wa wafanyabiashara hao  Bi.Fatma Ramadhani  amesema kuwa soko hilo halina paa hivyo wamekua  wakipata shida hasa majira ya mvua na kupelekea bidhaa nyingi kuharibika
Biashara  zinazopatikana  katika soko la kwa morombo jijini arusha.
Amesema bidhaa hizo ni nyanya,pilipili hoho pamoja na baadhi ya matunda huaribika kutokana na kunyeshewa na mvua mara kwa mara, pia amesema tatizo lingine ni kukosekana kwa wateja kipindi cha mvua kwa sababu ya matope yaliyopo sokoni hapo.
Pia ameendelea kusema manispaa imewataka kuhamia  soko la mnada lililopo jirani na eneo hilo na hawajaridhia kwa sababu eneo hilo limebadilika kuwa makazi ya watu hvyo kupelekea  eneo kuwa dogo hali ambayo haitoshelezi kuwa na bidhaa zao.hata hivyo  amesema soko ambalo wanashinikizwa kuhamia halina wateja kulingana na eneo walilopo sasa.
kwa upande  wa mwenyekiti wa eneo hilo Bw. Erastus Mwita amekiri kuwepo kwa katizo hilo na kuahidi kulishughulikia.

0 comments:

Post a Comment