Friday, February 14, 2014

Mgomo wa EFD waisha

Na Mariam George
 
]Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa jumuiya za wafanyabiashara wa kati wa Kariakoo na mikoani kuhusu mgogoro wa matumizi ya mashine za kielektroniki za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jijini Dar es salaam, juzi. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu  

 Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) imetangaza kusitisha mgomo wa wafanyabiashara uliodumu kwa takriban siku tano kupinga notisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kuwapa siku 14 za kufunga Mashine za Elektroniki za Kutoza Kodi (EFD).


Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Patrick Masagati alisema jana kuwa mgomo huo umefutwa baada ya makubaliano baina yao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda huku akisema kimsingi hawapingi matumizi ya mashine za EFD, isipokuwa mfumo mzima wa utozaji kodi nchini.
jana kuwa mgomo huo umefutwa baada ya makubaliano baina yao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda huku akisema kimsingi hawapingi matumizi ya mashine za EFD, isipokuwa mfumo mzima wa utozaji kodi nchini.
“Waziri Mkuu, Pinda amesitisha notisi ya TRA ya siku14 na ameahidi kuunda chombo kitakachopitia mfumo mzima wa kodi nchini,” alidai Masagati.

Hata hivyo, hakuna taarifa yoyote rasmi iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mazungumzo hayo na Mwandishi wake wa Habari, Irene Bwire hakupatikana pia kuzungumzia suala hilo.
Makamu huyo wa JWT alidai kuwa Waziri Mkuu aliahidi kuchukua hatua stahiki kwa haraka baada ya kukutana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya na watendaji wa TRA.
Masagati alisema katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa na wenyeviti wa jumuiya hiyo kutoka mikoani, pia walimfahamisha Waziri Mkuu kuhusu mianya ya rushwa ndani ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)  FROM mwananchi








0 comments:

Post a Comment