Friday, February 14, 2014

Profesa Kaisi: Daktari wa kwanza kuzalisha kwa njia ya upandikizaji

Na Mwajuma Abdul

 

 Profesa Kaisi: Daktari wa kwanza kuzalisha kwa njia ya upandikizaji 

 NI Daktari alieonyesha moyo wa kuendelea na kazi licha ya kupata maradhi ya kiharusi yaliyomsababishia kupooza mkono na mguu.
Hapana shaka kuwa maelfu ya wanawake nchini waliowahi kupata huduma zake wanamkumbuka bado kwa msaada mkubwa aliowapa na kuwasaidia kushika mimba, kuwapa ushauri wa kitaalamu au hata kuwazalisha.
Licha ya kustaafu, atabakia  kukumbukwa kwa mengi hapa nchini, hasa kwa mchango wake kwenye sekta ya afya ya mama na mtoto.
Huyu si mwingine, bali ni  Profesa Malise Kaisi, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi  ya Tiba (Muhas). Nafika nyumbani kwake maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam na ninamkuta akiwa amejipumzisha. Anaanza kwa kunipa historia  yake fupi ya  kikazi.

Atoa damu kuokoa wagonjwa
Nia ya daktari yeyote duniani, ni kuokoa maisha ya mgonjwa. Hiyo ndiyo faraja ya wataalamu wa afya walio wengi.
Akiwa ni daktari ambaye anaipenda kazi yake, Profesa Kaisi amewahi kujitolea damu kuwaokoa wagonjwa wake katika dakika ambazo pengine walikuwa kwenye bonde la uvuli wa mauti
.
“Unajua wakati ule, damu ilikuwa ni tatizo kubwa. Hakukuwa na benki ya damu kama ilivyo sasa, hivyo unapopata mgonjwa anayehitaji damu na yupo mikononi mwako, lazima ujitoe mhanga” anasema
Anakumbuka mwaka 1970 ambapo alimpokea mgonjwa aliyepata ajali mbaya na alihitaji damu. Ilibidi ajitolee damu yake ili kumwokoa mgonjwa yule.
“Nikiwa Newala mwaka 1970 huo huo, mgonjwa wangu aliyekuwa anajifungua aliishiwa damu sana na ikabidi nitoe damu yangu haraka sana na kumuwekea na alipona,” anasema
 Mara nyingine akiwa ndiyo kwanza ameripoti kwenye kituo kipya cha kazi huko Mtwara, alifika na kumkuta mgonjwa akiwa kwenye hali mbaya na hakuwa na mtu wa kumpa damu hivyo alikuwa akisubiriwa kufa, yeye alitoa damu yake na mgonjwa akapona.
“Cha muhimu ni kufahamu  kama una maambukizi au la. Ukishajijua, unatakiwa utoe damu kama wewe ni daktari,” anasisitiza Profesa Kaisi.

 CHANZO:MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment