Friday, February 14, 2014

Ukimwi kwa vichanga; changamoto kubwa kwa jamii

 Na Mwajuma Abdul

Mamia ya wanawake nchini wapo katika huduma ya kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Ni mapema asubuhi katika kibaraza cha Hospitali ya Wilaya ya Tanga iliyoko Ngamiani, makumi ya kinamama wajawazito wameanza kuchukua nafasi katika benchi la kuingia katika chumba cha ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya Ukimwi (VVU) kabla ya kuendelea na huduma nyingine za uzazi.
Kinamama hao ni tofauti na wengine ambao wameishafanya kipimo hicho ambao wamefika hapo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya hali zao na kadri muda unavyokwenda ndivyo idadi inaongezeka kila mmoja akiwa ametoka umbali wake ili kuifikia huduma ya kliniki.

Wanawake hao ni sehemu ya waelfu wengine ambao wanakusanyika katika vituo vya huduma za afya sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya huduma za kliniki ambako huko wanapimwa pia virusi vya Ukimwi na wapo ambao wanapata huduma ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Ripoti ya karibuni ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inabainisha kuwa kinamama wajawazito  69,937 waliokutwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi mwaka 2012, kati yao 44,799 walipata dawa ya kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto.
Idadi hiyo ni kwa wale wanawake wajawazito ambao wameandikishwa katika kliniki za mama na mtoto na ni tofauti na wale ambao hujifungulia nyumbani kwa wakunga wa jadi kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na umbali wa kukifikia kituo cha afya.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa mpango huo ambao umeanza kutekelezwa nchini toka 2011, umesaidia kupunguza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa asilimia 26 mwaka 2009 hadi asilimia 15 mwaka 2012.
Kiwango hicho hata hivyo kinatajwa kuwa kidogo na hakilingani na hali halisi na kufanya lengo la kufanya maambukizi kuwa kufikia asilimia 4 ifikapo 2015 kwani lengo hilo huenda lisifikiwe iwapo jitihada za maana hazitafanyika.
Ripoti hiyo ya wizara inabainisha kuwa asilimia 70 ya kinamama wajawazito nchini wapo katika tiba ya kuzuia maambukizi kwenda kwa watoto na huduma hiyo ambayo inatolewa kwa asilimia 94 na vituo vya afya ya uzazi.
Shirika la Umoja la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef), tawi la Tanzania  linaeleza kuwa ni asilimia 50 pekee ya watoto wanaozaliwa ndio wanapata huduma ya kupima virusi vya Ukimwi na ni asilimia hiyo pia ya wajawazito wengi nchini hufika mara nne kliniki katika kipindi cha ujauzito wao hali ambayo inafanya usimamizi kuwa usio na mtiririko.
Pia, unyanyapaa ni sababu nyingi inayofisha mapambano dhidi ya mpango wa kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Masula ya Afya la Pharm Access, Geert Haverkamp anabainisha umuhimu wa huduma hiyo katika kufikia lengo la kuhakikisha hakuna maambukizi mapya

Chanzo:MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment