Wednesday, February 26, 2014

Afrika Kusini yasema itawalinda mashoga dhidhi ya ukatili

Serikali ya Afrika Kusini imesema itazuia ukatili dhidi ya watu wenye uhusiano wa jinsia moja Msemaji wa wizara ya uhusiano wa kimataifa na ushirikiano Bw Clayson Monyela amesema, serikali ya Afrika Kusini itahakikisha kuwa vitendo vya ukatili vitaadhibiwa, na wahusika watachukuliwa hatua, kukamatwa, kufungwa na kuhukumiwa.

Mwaka 1996 Afrika Kusini ilikuwa nchi ya kwanza duniani inayotoa ulinzi wa kikatiba kwa watu wenye uhusiano wa jinsia moja. Nchi hiyo pia ni nchi pekee barani Afrika inayotambua ndoa ya jinsia moja.
     From IDHAA YA CHINA KIMATAIFA
Na Albariki Madihi

0 comments:

Post a Comment