Tuesday, February 25, 2014

KUKIDHIRI KWA TAKATAKA KATIKA ENEO LA SOKO

LOCAL STORY
NA MARYLINE .D. OLOTU

Wafanya biashara wa soko la kwa mrombo, wamelalamikia halmashauri ya wilaya ya Arusha kwa kushindwa kuthibiti tatizo la uchafuzi wa mazingira sokoni hapo.

Akizungumza na idhaa hii mfanya biashara wa matunda John Hamisi na Halima Saidi,anayejishuhulisha na biashara ya mboga,amesema tatizo la uchafuzi wa mazingira sokoni hapo  limekuwa sugu kwani wametafuta ufumbuzi wake bila mafanikio.

Uchafu uliorundikana katika eneo la soko hilo

Pia wamejaribu kufikisha malalamiko yao kwa viongozi wa mtaa wa eneo hilo,kwa halmashauri ya wilaya ya Arusha mjini lakini viongoz hao wameshindwa kuwatatulia tatizo hilo.

Aidha waliendelea kwa kusema kuwa,wanaitaka halmashauri hiyo kuacha kukusanya kodi kwani hawaoni matunda ya kuenselea kulipa kodi zao kwani mazingira wanayofanyia biashara hayaridhishi na ni hatarishi kwa afya zao.
baadhi ya wafanya biashara wakiendelea kufanya biasha na huku wakizungukwa na uchafu


Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia mazingira ya soko hilo yakiwa machafu huku wafanya biashara wakiendelea na shughuli zao za kila siku.

Baadhi ya wanunuzi wamesema hali hiyo ni hatari kwa afya zao kwani wanaweza kuugua magonjwa hatarishi ya mlipuko ikiwemo kipindu pindu
Hali ya urundikwaj wa taka katika soko la kwa mrombo Arusha.
 
Jitihada za kuutafuta uongozi wa halimashauri hiyo ya jiji la Arusha ziligonga mwamba kwani simu zao zilikuwa zikiita bila mafaniko yoyote na hazikupokelewa.

0 comments:

Post a Comment