Wednesday, February 26, 2014

UWIZI ARUSHA STENDI



Abiria wanao ingia na kutoka katika mkoa wa arusha wameuomba uongozi wa mkoa kuweka utaratibu mzuri katika stendi ya mkoa ili kuepusha zoezi la abiria hao kuibiwa mizigo yao.
Hayo yamesemwa na baadhi ya abiria katika stendi hio, ni kutokana na msongamano wa makondakta wanao pigia debe mabasi mbalimbali yanayo ingia na kutoka katika stendi hio.
Kwa mujibu wa baadhi ya makondacta wanao patikana katika stendi ya mkoa wa Arusha wamedai kwamba tabia ya wizi katika stend hiyo inasababishwa na watu wengine haswa wanao jifanya wabeba mizigo na matoroli sambamba na makondacta walio feki.

 Na Albariki madihi

0 comments:

Post a Comment