Tuesday, February 25, 2014

















wakazi wa mtaa maua kata ya arusha mjini,wameitaka serikali ya halmashauri ya mji  wa Arusha kuwajengea kwa kiwango cha lami,barabara ya mbauda inayounganisha mtaa huo na barabara kuu ya kwa morombo.

wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari,wakazi wa mtaa huo walisema licha ya barabara kutumiwa na magari makubwa ya kusafirisha mizigo kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi,lakini hawajaikarabati hali ambayo inawapa wakati mgumu watumiaji wa barabara hiyo wakufanya kazi zao kwa wakati,kutokana na barabara hiyo kujaa mashimo.

Venance kilasi alisema licha ya kuwa eneo la mtaa huo ni miongoni mwa maeneo yanayotegemewa na halmashauri ya mji wa arusha katika kuingiza mapato ya ndani,lakini imekuwa haipei kipaumbele cha lami na kuongeza kuwa kwa muda mrefu sasa barabara hiyo haijafanyiwa ukarabati.

Barabara hii inatumika sana kwa kusafirisha mizigo na kuipatia halmashauri kipato,lakini haipewi kipaumbele cha kuwekwa lami alisema kilasi naye benjanibi mlowe alisema serikali imezoea maafa ndio maana kwa sasa inajifanya haioni barabara hiyo ilivyoharibika,yakitokea maafa ndio wanajifanya wanaitengeneza kwa sasa wasafiri wanapata shida sana kwa kukwama.

Mwenyekiti wa mtaa wa maua elirehema matinya alisema walishaandika barua ya kuiomba halmashauri kuwajengea barabara huyo kwa kiwango cha lami lakinki mpaka sasa utekelezaji wake bado unasumbua.

khadija omary.

0 comments:

Post a Comment