Tuesday, February 25, 2014

KUPUNGUZIWA KWA KODI KWA WAMILIKI WA BODABODA


Madereva wa usafiri aina ya bodaboda Mkoani Arusha eneo la kwa Morombo wameiomba serikali kuondoa kodi kwa wamiliki wa vyombo hivyo.

Hayo yamesemwa na mmoja wa madereva hao Bw.Mosiri Mnono wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari kituoni hapo eneo la kwa Morombo.

Bw.Msori Mnono amsema kua kodi inayotozwa na Serikali ni kubwa kulingana na kipato wanachokipata hali inatowasababishia kutokulipwa vizuri na wamiliki wa vyombo hivyo.

Ameendelea kwa kuema kuwa Serikali imekuwa ikiwanyonya ikiwa ni pamoja na kuwatoza fedha nyingi pindi wanapokuwa wakifanya kazi zao wakati bado wanafanya
kazi katika mazingira magumu.
.
.''Hii serikali kweli imtuchosha wanatutoza kodi sawa na wamiliki wa magari wakati hivi ni vyombo tofauti na mapato hayalingani wamshatufanya sii ni shamba la bustani''Alisema Mnono

Madereva hao wa bodaboda wameiomba serikali kuwaondolea malipo ya kodi kwa wamiliki ili na wao wanufahike na kazi wanayoifanya ambayo pia imeisaidia serikali kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.
Na Mwandishi Wako
Lightness urassa Arusha

0 comments:

Post a Comment