Tuesday, February 18, 2014

WACHIMBAJI HARAMU WAFIKISHWA KIZIMBANI

NA:MARIAM  HASSAN

 Kundi la wachimbaji migodi haramu waliookolewa kutoka mgodi uliotelekezwa nchini Afrika Kusini na maafisa wa uokoaji wanatarajiwa kufika kizimbani hivi leo.

Wachimbaji migodi hao 11 walitumia ngazi iliyotupwa ndani ya mugodi huo kujinasua siku ya jumatatu.
Wote 22 walikamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Vyombo vya habari vya Afrika Kusini vinasema takriban wachimba migodi wengine 200 bado wamenasa katika mgodi huo lakini wamekataa kuokolewa wakihofia kukamatwa na polisi. Baadhi yao wanatoka katika mataifa jirani

CHANZO:BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment