Na Amalia seraphine
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema Simba wamekurupuka
katika suala la Emmanuel Okwi.
Manji ameiambia kwamba Simba wamefanya haraka kumsajili
mchezaji ambaye ana mkataba na Yanga.
“Okwi bado ni mchezaji wa Yanga, ana mkataba na Yanga lakini
ana kesi na Yanga.
“Simba wamekiuka sheria za Fifa kwa kumsajili mchezaji
ambaye ana mkataba. Sisi tumemfungulia Okwi mashitaka akiwa bado mchezaji wetu
na mkataba wetu naye haujaisha.
“Sasa walishindwa hata kutuuliza kuliko kukurupuka hivi,”
alihoji Manji.
“Leo nitazungumza na waandishi, unaweza ukanisikiliza na
kupata ninachosema lakini nakuhakikishia Simba wamekurupuka na wamevunja sheria
na kanuni za Fifa kumsajili mchezaji mwenye mkataba na mtu mwingine.
“Sikuona sababu ya wao kujiingiza matatizoni,” alisema Manji
ambaye anazungumza na waandishi leo saa tano asubuhi kuhusiana na suala hilo la
Okwi.www.LAKE NATRON CLASS.BLOGSPOT.COM
0 comments:
Post a Comment