Tuesday, February 25, 2014

Baadhi ya wananchi wa kata ya Sombetini wakiwa kwenye foleni ya maji.
NA PENDO MICHAELI

Ukarabati wa barabara katika kata
ya Sombetini jijini Arusha umesababbisha ukosefu wa maji katika eneo hilo.

Akiizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wanachi hao bi. Frida Malia amese tatizo hili limedumu kwa muda wa mwezi mmoja hivi sasa hali inayowalazimu kufuata maji kwa umbali mrefu.
Ameendelea kusema hali hiyo inawapa shida hasa katika kipindi hiki cha mvua kwani watoto wamekuwa wakichelewa kwenda shule kwa ajili ya kufuata maji hivyo kukosa vipindi vya asubuhi.
Kwa upande wake kiongozi wa eneo hilo Bw. Alli Said amekiri kuwepo kwa tatizo hili katika eneo lake na haidi kulishughulika tatizo hili.
Aidha amewaomba wanachi kuwa wavumulivu katika kipindii hiki kigumu kwani mabomba yatatengenezwa pindi ukarabati wa barabara utakapo kamilika.

0 comments:

Post a Comment