Monday, September 1, 2014

VIKOSI VYA USALAMA VYAPAMBANA NA AL-SHABAB SOMALIA..

Vikosi vya usalama vya Somalia vimezima shambulio la wanamgambo wa al Shabab katika makao makuu ya masuala ya kiintelijinsia na kitengo cha mahabusu huko Mogadishu mji mkuu wa nchi hiyo.

 Polisi na watu walioshuhudia wameeleza kuwa shambulio hilo la leo lilianza baada ya kulipuka gari lililokuwa limetegwa bomu nje ya kituo cha taifa cha masuala ya intelijinsia, mlipuko uliofuatiwa na shambulio la watu wenye silaha waliovalia sare za jeshi la taifa la Somalia.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Somalia amesema kuwa mmoja wa wavamizi ameuawa kwenye mlipuko wa bomu na wengine sita wameuliwa na vikosi vya usalama.  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Somalia ameongeza kuwa shambulio hilo limekwisha na kwamba wavamizi wameshindwa kutimiza lengo lao la kuvuruga oparesheni ya bahari ya Hindi akiashiria oparesheni ya nchi kavu inayotekelezwa sasa na Umoja wa Afrika na serikali ya Somalia. Wakati huo huo Msemaji wa kundi la al Shabab Abdulaziz Abu Musab amethitibitisha shambulio hilo na kudai kuwa wanamgambo wao wamewaua maafisa kumi wa usalama na kuwaachia huru mahabusu kadhaa.



Habari na Theodora Massawe
Chanzo:BBC

0 comments:

Post a Comment