Aliyeva shati jeupe ni Waziri Emmanuel Ndenshau kiongozi wa hosteli za Loliondo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha akihojiwa na mwandishi wa blog hii Gift Adison.picha na TEODORA MASSAWE.
Baadhi ya wanafunzi wa hosteli wakiwa katika eneo la kantini..picha na TEODORA MASSAWE.
Baadhi ya wanafunzi wa hosteli wakiwa wanajisomea katika eneo la hosteli..picha na TEODORA MASSAWE.
Habari na GIFT ADISON,
Wanafunzi wa
chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha wanaoishi hosteli za loliondo
wameomba uongozi wa hosteli hiyo kuwapatia vifaa vya kufanya usafi kwa wakati
ili kuweka mazingira safi.
Wakizungumza
na waandishi wa habari mapema leo wamesema kuwa wamekuwa wakicheleweshewa vifaa
vya kufanya usafi kitendo kinachowapelekea mazigira ya hosteli hiyo
kotoridhisha.
Mmoja kati
ya wanafunzi hao aliyejitambulisha ZIARA NYATU amesema kuwa maisha ya hosteli
ni mazuri endapo mazingira yatakuwa safi ili kuwaepusha na magonjwa ya milipuko
kama vile kipindupindu
``Maisha ya hositeli yananisaidia kuwa huru
kitaaluma kwani nakuwa na muda mwingi wa
kubadilishana mawazo na wezangu na
kufanya mazoezi ya vitendo katika kituo cheti cha redio hapa chuoni ``Alisema
nyatu.
Pia ameeleza changamoto wanazokabiliana
nazo kuwa ushirikiano hafifu kwa
wanafunzi wengine kawa kutoshiriki katika ufanyaji usafi, tabia ya wizi, uhaba
wa maji safi ya kunywa, na pia kuwapelekea baadhi ya wanafunzi kuzidi kuhama
kutoka katika hosteli
``wanafunzi
wengi wanatoka sehemu mbalimbali kila mtu akiwa na tabia yake hivyo inachukua
mda kumbadilisha mtu kuendana na mazingira Fulani ambayo hajayazoea kama vile
kufannya usafi wa jumla, na kuchoma taka pale zinapoonekana kujaa`` alisema nyatu
Kwa upande wa kiongozi wa
hosteli ya loliondo bwana Emmanuel Ndanshau amesema kuwa amekuwa akifanya
vikao chumba hadi chumba ili kuweza
kuwashauri na kuwaonya pale wanapokwenda kinyume sheria na utaratibu wa hosteli
Bwana Ndanshau ameeleza
matatizo anayokumbana nayo katika mazingira hayo ni gari la taka kuchelewa
kufika kwa wakati pamoja na uhaba wa maji safi ya kunywa ingawa maji
yanayopatikana ni ya kisima kwani sio bora kwa afya zao
0 comments:
Post a Comment