TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Leo asubuhi, Ijumaa, Machi 14, atamwapisha Katibu wa Baraza la
Wawakilishi Bwana Yahya Khamis Hamad kuwa Katibu wa Bunge Maalum la
Katiba.
Aidha,
katika sherehe fupi itakayofanyika Ikulu Ndogo, Dodoma, Rais Kikwete
atamwapisha Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Thomas Didimu Kashililah kuwa Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.
Taarifa
iliyotolewa Jana jioni , Alhamisi, Machi 13, mwaka huu wa 2014 mjini
Dodoma na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa Rais
Kikwete atawaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba
kwa mujibu wa kifungu cha 24(7) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura
ya 83, toleo la mwaka 2014.
Bwana Hamad na Dkt. Kashilillah
wanashika nafasi hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 24(1) cha Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, toleo la mwaka 2014, ambacho kinasema
kuwa nafasi za Katibu na Naibu katibu wa Bunge Maalum la Katiba
zitajazwa na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar.
Kwa mujibu wa kifungu cha 24(3) cha
sheria hiyo, Sura ya 83, toleo la mwaka 2014, Katibu wa Bunge Maalum
atatoka upande tofauti na ule anakotoka Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
Kwa vile aliyechaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Mheshimiwa Samuel John Sita anatoka Tanzania
Bara, basi Katibu wa Bunge anakuwa Bwana Yahya Khamis Hamad ambaye ni
Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar na Naibu Katibu wa Bunge
Maalum la Katiba anakuwa Dkt. Kashililah ambaye ni Katibu wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
0 comments:
Post a Comment