Bibi mmoja nchini Mexico amefanikiwa
kuhitimu elimu ya shule ya msingi akiwa
na umri wa miaka 100.
Bibi huyo Manuela Hernandez (pichani)
ambaye alizaliwa katika jimbo la Oaxaca
mnamo mwezi Juni 1913, aliacha shule ya
msingi baada ya kusoma kwa mwaka
mmoja tu na kurejea kuisaidia familia
yake masikini kufanya kazi za nyumbani.
Hata hivyo alirejea shule kuendelea na
masomo mwezi Oktoba mwaka uliopita
akiwa na miaka 99 kufuatia kushauriwa
na mmoja wa wajukuu zake.
Manuela Hernandez akiwa ameshikiliacheti chake cha kuhitimu elimu ya
msingi.Hivi sasa tayari amekabidhiwa diplomayake ya elimu ya msingi
katika shereheiliyofanyika katika jimbo Mexico Kusini.Bibi Hernandez
amesema sasa ataendeleana masomo ya elimu ya sekondari.Zaidi ya nusu ya
wakazi wa jimbo laOaxaca wenye umri wa zaidi ya miaka 15hawajamaliza
elimu ya msingi.
0 comments:
Post a Comment