Thursday, March 20, 2014

Mahakama yaruhusu Mkenya kufikishwa ICC



wakili wake Kibe Mungai kushindwa kufika mahakamani ili kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Hatua hiyo inamaanisha kwamba waziri wa usalama nchini Kenya Joseph Ole Lenku anaweza kuomba agizo la
kukamatwa kwa mwandishi huyo kabla ya kuwasilishwa katika mahakama ya ICC anakotakikana.
Walter Baraza anatakikana na mahakama hiyo kwa madai ya kuingilia ushahidi katika kesi inayomkabili makamu wa rais
wa kenya William Ruto.
Uamuzi wa Jaji wa Mahakama Kuu Richard Mwongo ni pigo kubwa kwa Mwandishi wa habari Walter Barasa, ambaye
alikuwa aking'ang'ana kuhakikisha kuwa hakamatwi na kusafirishwa hadi Hague kushtakiwa kwa kosa la kuwaingilia
mashahidi waliokuwa wameorodheshwa na kiongozi wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.
Mwaka uliopita Kiongozi wa mashtaka katika The Hague, Fatou Bensouda, alitoa ombi ambalo lilikubaliwa na
kuwasilishwa nchini Kenya ambapo ilitakiwa Waziri wa Maswala ya Usalama Nchini Kenya Joseph Ole Lenku, amkamate
na kumfikishakatika The Hague.
Katika agizo hilo ilidaiwa kuwa Bwana Barasa alitumia pesa kuwahonga mashahidi waliotarajiwa kutoa ushahidi dhidi
ya Naibu Rais wa Kenya, William Ruto na mtangazaji Joshua arap Sang.
Wakenya hao wawili wameshtakiwa kuwa walichangia pakubwa katika kuchochea ghasia za baada ya Uchaguzi wa
mwaka 2007 na 8, ambapo zaidi ya watu 1,300 waliuawa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe baada ya
upande wa upinzani kupinga matokeo ya uchaguzi.
Tangu kutangazwa kuwa akamatwe Baraza alikanusha kuwa alihusika katika njama hiyo na akadai kwamba Mahakama
ya Kimataifa ilikuwa ikitaka kumgandamiza tu kwa sababu yeye alikataa kujitolea kutoa ushahidi dhidi ya Bwana Ruto
na mwenzake Bwana Sang.
Awali Jaji Mwongo alikuwa ametoa amri kuwa Baraza akamatwe na kupelekwa Hague lakini Wakili wa Bwana Baraza
Kibe Mungai, akaomba utekelezaji wa uamuzi huo uahirishwe ili yeye, Bwana Kibe ajitokeze mahakamani kutoa
ushahidi kwa nini Bwana Baraza asikamatwe.
Wakili Kibe alitarajiwa kuwasilisha sababu zake jana lakini hakuwepo, jambo ambalo lilimlazimisha jaji kurejesha amri
ya awali kuwa Baraza akamatwe.
Tangu mashtaka kuwasilishwa dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, naibu wake William Ruto na Bwana Sang katika
Mahakama ya Kimataifa mashahidi wengi wamejiondoa kutoa ushahidi wakidai kuwa wanatishwa ingawa Bi Bensouda
kwa upande wake anasema wengi wao wanahongwa na wandani wa washtakiwa.

0 comments:

Post a Comment