Rais Uhuru Kenyata akitafakari jambo
Shangazi
wa Rais Uhuru Kenyatta amekuwa moja wapo wa waathiriwa wa wizi wa
magari kwa kutumia nguvu nchini Kenya, baada ya kushambuliwa na kuibiwa
gari lake akiwa katika msongamano wa magari kwenye njia kuu ya Uhuru.
Watu
watatu walokuwa na bunduki walingia kwa nguvu ndani ya gari la Bi.
Njeri Muhoho, mwenye umri wa miaka 56, na kumzungusha katika jiji la
Nairobi kwa karibu saa mbili kabla ya kumshusha karibu na shule moja ya
kimataifa katika mtaa wa kaskazini wa Gigiri.
Bi.
Muhoho, ambae ni mke wa mkuu wa zaamani wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
vya Kenya, George Muhoho, aliwambia polisi kwamba alikua garini pamoja
na mwanamume mwenye umri wa miaka 25 wakati gengi la watu watatu
walipowashambulia Jumanne, saa mbili na nusu usiku.
Polisi
wanaeleza kwamba walishambuliwa wakiwa wanasubiri taa ya kuongoza
magari kubadilika kuwa kijani, na aliibiwa Sh 20,000 za Kenya, pamoja na
kadi yake ya benki ATM, na leseni ya kuendesha gari.
Mkuu
wa polisi mjini Nairobi Benson Kibue anasema baada ya kuwashusha, wezi
hao watatu walelekea mahala isipojulikana na gari lao la aina ya Nissan.
Msako unafanyika kutafuta gengi la watu hao
Friday, March 14, 2014
SHANGAZI WA RAIS KENYATA ATEKWA JIJINI NAIROBI
1:46 AM
No comments
0 comments:
Post a Comment