Tuesday, September 9, 2014

WANAFUZI WA AJTC WAASWA KUWA NA MWITIKIO KWENYE MASHINDANO YA UTANGZAJI

Mkuu wa idara ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaziji arusha bwana Onesmo Elia Mbise akifanya  maojiano na mwanishi wetu (picha na mwanaidi omary)


Mkuu wa idara ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaziji arusha bwana Onesmo Elia Mbise amewaasa wanafunzi wa chuo hicho kuwa na mwitukio pindi yanapotokea katika mashindano ya utangazaji
Amesema dhumuni la mashindano hayo ni kuinua vipaji vya utangazaji  na kuimarisha wanafunzi katika uandaji wa vipindi wa radio na Tv
“Dhumuni la mashindano haya ni kuinua vipaji vya utangazaji kwa wanafunzi lakini pia kuimarisha wanafunzi katika uandaaji wa vipindi vya radio na runinga”
Ameendelea kusema kuwa utaratibu wa madarasa yote kushiriki  washiriki kutokuwa na muundo wa kuigiza chuoni hapo kubadilikabadilika  huku madarasa 13 kati ya 16 yakishiriki mashindano hayo huku madarasa 2 wiki moja maalumu ya utagazaji  kwa kuwa muda wao wa likizo unakaribia
Bwana onesmo amebainisha kuwa changamoto nyingi zinasababishwa na wanafunzi wenyewe kutokuwa na mwitikio  na wengine kutopenda kujitoa kwa sababu ya uoga
“Changamoto hazipo kwa upande wa idara ya utangazaji bali zipo kwa wanafunzi wenyewe kutokuwa na mwitikio na kutopenda kujitoa kwa sababu ya aibu” alisema bwana Onesmo
Alimalizia kwa kusema wanafunzi wategemee makubwa kwa mashindano yanayofuata kwa kuwa yatakuwa na sehemu mbili ya kwanza ni mashindano yatakayofanyika chuoni hapo na sehemu ya pili ni mashindano  na vyuo vingine vitano vilivyopo arusha . HABARI NA AMALIA SERAPHINE 

0 comments:

Post a Comment