Monday, September 1, 2014

ujerumani kuwapatia sila wakurd


Ujerumani inatarajia kulitumia jeshi la Wakurd wa Iraq silaha ikiwemo bunduki na silaha zile zenye mfumo unaoweza kukabiliana na mashambulizi ya vifaru vya kivita.
Jeshi hilo limekuwa likipambana na wapiganaji wa kiislamu kaskazini mwa Iraq.

Amesema uamuzi huo ni kutokana na maslahi ya nchi yake.Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula Von der Leyen amesema silaha hizo zotaweza kuwatosheleza wanajeshi elfu nne ifikapo mwishoni mwa Septemba.
Hatua hiyo iliyochukuliwa na Ujerumani imeelezwa kuwa ni ya nadra sana kwa nchi hiyo, kupeleka silaha kwenye eneo lenye mapigano.
Hata hivyo uamuzi huo umekosolewa na baadhi ya watu ambao wana wasiwasi zitakapoishia silaha hizo.                                                                                                 na mwandishi wako kennedy rutta

0 comments:

Post a Comment