Afisa mahusiano na masoko katika chuo cha uandishi
wa habari na utangazaji Arusha A.J.T.C Bw. Israeli Mungure amesema mahusiano baina
ya chuo na majirani yameboreshwa kwa kuzingatia sheria na taratibu.
Kulia:Afisa mahusiano na masoko katika
chuo cha uandishi wa habari Arusha akizungumza na mwandishi wa blogu hii Steven
Mulaki. (Picha na Winlady Johaness)
Akizungumza na mwandishi wa habari wa blogu hii bwana
Mungure ameeleza njia mbalimbali ziliotumika ikiwamo njia ya kuzungumza na
majirani wanaozunguka chuo hicho.
Aidha bwana Mungure amebainisha tabia waliokuwa nazo
baadhi ya wanafunzi hasa wa kike ikiwa na pamoja na kuvaa mavazi yaliwakwaza
majirani wa chuo hicho.
TUMEBORESHA MAHUSIANO
CHUONI: Bwana Israeli Mungure kieleza kuhusu uboreshaji wa mahusiano katika
chuo cha habari Arusha. (Picha na Winlady Johaness)
Hata hivyo Israeli Mungure ameeeleza hatua walizochukua ni pamoja na
kuwaadhibu wanafunzi wanaovunja maadili hasa kwa kuvaa nguo fupi
zinazowapelekea majirani kuwa na hofu.
Vilevile bwana Mungure ameelezea uhusiano baina ya
wafanyakazi wa chuo hicho na kusema kwa
sasa umeboreshwa kwa kuwa wote hufanya kazi kwa ushirikiano.
Kwa upande wao wanafunzi wa chuoni hapo wameeleza
kuridhishwa na mahusiano yaliyopo baina yao na walimu pamoja na majirani
wanaozunguka chuo hicho.
Kulia:Mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa
habari Arusha Theodora Massawe akizungumza na mwandishi wa blogu hii Steven
Mulaki. (Picha na Winlady Johaness)
Kadhalika mmoja wa wanafunzi bi Theodora Massawe
amewaasa wanafunzi wenzie kuwa na nidhamu na kufanya yale yaliyowapeleka chuoni
hapo.
Kwa upande wake Afisa Mahusiano wa chuo hicho
amezitaja changamoto anazokumbana nazo katika kazi zake ikiwemo changamoto ya
kuwaelewesha majirani juu ya taratibu na sheria za chuo hicho.
Aidha kwa wale majirani waliolalamikia suala la kuchota
maji bwana Mungure amewatoa
wasiwasi kwa kusema kuwa umepangwa muda
maalumu wa kuteka maji chuoni hapo ikiwa ni kuanzia saa kumi jioni mpaka saa
kumi na mbili jioni.
Bwana Israeli Mungure amewasihi wanafunzi kuwa
makini katika masomo na kuzingatia taaluma yao inahitaji ualedi na nidhamu ya
hali ya juu.
0 comments:
Post a Comment