Monday, September 1, 2014

Putin aelekeza shutuma Ukraine Mashariki


habari EVALIYNE BAKARI
Mwanaharakati wa demokrasi aliyetuhumiwa na wapiganaji kuwa jasusi wa serikali ya Ukraine, apigwa teke na mpita njia na kuzomewa mjini Donetsk
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametoa wito kufanywe mazungumzo ya haraka kuhusu uhuru wa mashariki mwa Ukraine, kama sehemu ya mazungumzo ya kumaliza vita vya huko.
Bwana Putin amenukuliwa akisema kuwa "masilahi ya haki" ya watu wanaoishi katika jimbo hilo lazima yalindwe.
Mwandishi wa BBC anasema matamshi ya Rais Putin ni ishara kuwa Urusi inataka serikali ya Ukraine izungumze moja kwa moja na wapiganaji wanaoipendelea Urusi, kuhusu amani.
Urusi ina hamu ya kuongoza mchakato huo.
Rais Putin amesema hayo siku moja kabla ya mazungumzo kuanza mjini Minsk, Belarus ( nchi jirani na Ukraine) baina ya Ukraine, Urusi na Umoja wa Ulaya, kujadili msukosuko huo.
Na Umoja wa Ulaya na serikali ya Ukraine wameonya kuwa hali katika eneo hilo inakaribia kufika kiwango ambapo hali ya zamani haitoweza kurejeshwa tena.
Na katika tukio jengine Ukraine imekabidhi askari 10 wa miamvuli kwa Urusi, na Urusi imewarejesha wanajeshi 63 wa Ukraine.

0 comments:

Post a Comment