Mwanafunzi Eveline Molel[Kulia], akifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa blog hii Evelyine Bakari[kushoto]katika moja ya darasa ndani ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.picha na YASINTA PETER.
Mwanafunzi Yusuph Mbata Akijisomea Kujiandaa na Mtihani,picha na YASINTA PETER
Habari na EVELYINE BAKARI
Wanafunzi wa darasa la Ruaha katika
chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Arusha wanatarajia kufanya mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza kuanzia tarehe
15 mpaka tarehe 19 mwezi wa tisa mwaka huu.
Wakizungumza na AJtc
mapema jana wanafunzi hao wamesema kuwa wamejiandaa vizuri na mitihani
na wanatarajia kufaulu vizuri katika masomo yote, akizungumzia suala hilo
mwanafunzi wa darasa hilo Evelyn Mollel alikuwa na haya ya kusema,
‘’Nimejiandaa
vizuri na mtihani ambao tutaanza tarehe 15 mpaka tarehe 19 na ninatazamia
kufaulu vizuri katika masomo yote na nina hakika na wanafunzi wenzangu wamefanya hivyo.
Kuhusu suala
la mtaala mpya wanafunzi hao wamesema ,mtaala huo ni mzuri kwa kuwa unawawezesha
kujua na kupata muongozo wakati wanasoma pindi wanapokaribia kufanya mitihani
kwa kuwa wanasoma mitihani waliyopewa madarasa mengine hivyo hawapati shida
kufikiria wapi pa kusoma.
Wakielezea changamoto wanazokumbana nazo kuwa
ni pamoja na ukosefu wa ushirikiano kati ya wanafunzi wa darasa hilo na wengi
wao kutoroka darasani kabla ya muda wa kuondoka pamoja na kubadilishiwa tarehe
ya kufanya mtihani.
Pia
wanafunzi hao wamemalizia kwa kuwaasa wanafunzi wenzao wa madarasa mengine kusoma kwa bidii na waache mambo mengine na
kuzingatia masomo.
0 comments:
Post a Comment