Wednesday, September 10, 2014


WAJASIRIAMALI WADOGO KATIKA SOKO LA KWA MROMBO WAMELALAMIKIA UONGOZI WA SOKO HILO KUTOKANA MFUMUKO WA BEI.









(Kutoka kushoto ni mjariliamali MAMA ABDULY akizungumza na na mwaandishi wa habari mapema jana)

Mmoja wa wa mfanya biashara katika soko hilo aliyejulikana kama ,MAMA ABDULY akizungumza na waandishi wa habari hapo jana  katika sokoni hapo nakusema kupanda kwa bei za nyanya pamoja na mboga ni changamoto kwao kwani wanashindwa kukidhi mahitaji yao pamoja na familia zao

Alisema kuwa wamekuwa wakinunua sanduku (tenga) moja kwa bei ya shilingi eilfu tisa(9000) mpaka eilfu ishirini na mbili(22000) lakini kwa sasa wananunua kwa shilingi (25000) mpaka sh.30000 kwa bei ambayo inaleta changamoto wakati wakuwauzia wateja wao kwani wanashindwa kuelewana.

"Mteja aliyezoea kununua nyanya kwa bei nafuu alafu anakuta bei imepanda  mpaka kumuelewesha inachukua mda kwa sababu anakuta nyanya za mia tano ni nne(4) na amezoea kwa kukuta ni nyanya sita au saba anashindwa kuelewa" alisema mama abduly.

Aidha mjasiriamali huyo aliweza kuzungumzia biashara nyingine ya mboga  kwani wakulima walikuwa wanawauzia mboga fungu moja sh.100 lakin sasa wanawauzia fungu 3 kwa shilingi mia tano.(500) bei ambayo ni kikwazo kwao.

"kama unavyoona sijasoma sana na nimeamua kujishughulisha na biashara hii ya uuzaji wa nyanya na mbogamboga kwa kukidhi mahitaji yangu       pamoja na familia yangu pia nasomesha watoto kupitia biashara hii,nimenunua kiwanja kupitia biashara hii ambapo ni faida nayoipata lakini sasa nashindwa  kupta faida kutokana na bei hizikabisa",alisema

Pamoja na hayo wafanya biashara hao wameendelea kusema kuwa 
changamoto hizo zinaambatana nakutokuwepo kwa choo,maji kwani ni huduma muhimi sanak wa jamii pamoja na sehemu maalum ya kufanyia biashara hizo kwani eneo hilo ambalo ni wanalitumia kwa sasa limekuwa dogo kutokana kuwa na wafanya biasharakatika eneo hilo.

Pia wafanya biashara hao walimazia kwa kusema wanauomba uongozi wa soko hilo kuwatengea eneo maalum kwa ajili ya biashara hiyo kwani eneo hilo wnaolifanyia biashara ni changamoto kwao na dogo sana kwani eneo hilo liko kandokandona barabara ikiwa nia hatari kwa maisha yao..HABARI NA ELIZABETH NJAU,PICHA NA GEORGE HILONGA



0 comments:

Post a Comment