Monday, March 31, 2014
MTIZAME BIBI WA MIAKA 100 AHITIMU ELIMU YA MSINGI!!!!!!!!!!!!
2:03 AM
No comments
Bibi mmoja nchini Mexico amefanikiwa
kuhitimu elimu ya shule ya msingi akiwa
na umri wa miaka 100.
Bibi huyo Manuela Hernandez (pichani)
ambaye alizaliwa katika jimbo la Oaxaca
mnamo mwezi Juni 1913, aliacha shule ya
msingi baada ya kusoma kwa mwaka
mmoja tu na kurejea kuisaidia familia
yake masikini kufanya kazi za nyumbani.
Hata hivyo alirejea shule kuendelea na
masomo mwezi Oktoba mwaka uliopita
akiwa na miaka 99 kufuatia kushauriwa
na mmoja wa wajukuu zake.
Manuela Hernandez akiwa ameshikiliacheti chake cha kuhitimu elimu ya
msingi.Hivi sasa tayari amekabidhiwa diplomayake ya elimu ya msingi
katika shereheiliyofanyika katika jimbo Mexico Kusini.Bibi Hernandez
amesema sasa ataendeleana masomo ya elimu ya sekondari.Zaidi ya nusu ya
wakazi wa jimbo laOaxaca wenye umri wa zaidi ya miaka 15hawajamaliza
elimu ya msingi.
WARIOBA AMCHANA LIVE PROF. SHIVJI
2:01 AM
No comments
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa gazeti hili,
nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi.
“Shivji alikuwa anasema Tanganyika imejificha kwenye Muungano ili inufaike. Kwa hiyo anasema Tanganyika iwe wazi isijifiche,” alisema Jaji Warioba.
DAR ES SALAAM.
MJADALA wa Mabadiliko ya Katiba jana ulihamia nje ya Bunge wakati Jaji Joseph Warioba alipomchambua mhadhiri maarufu nchini, Profesa Issa Shivji akimueleza kuwa si mkweli bali mpotoshaji wa Rasimu ya Katiba.
MJADALA wa Mabadiliko ya Katiba jana ulihamia nje ya Bunge wakati Jaji Joseph Warioba alipomchambua mhadhiri maarufu nchini, Profesa Issa Shivji akimueleza kuwa si mkweli bali mpotoshaji wa Rasimu ya Katiba.
“Shivji alikuwa anasema Tanganyika imejificha kwenye Muungano ili inufaike. Kwa hiyo anasema Tanganyika iwe wazi isijifiche,” alisema Jaji Warioba.
Wednesday, March 26, 2014
Monday, March 24, 2014
EXCLUSSIVE!!!!!! HUYU HAPA YULE MTOTO ALIYEOTA NYAMA ZA AJABU MWILINI KAMA PEMBE..... maombi yako ni muhimu
5:12 AM
No comments
HAKIKA UKIFANYA HIVI MUNGU ATAKUBARIKI KUWA NA HURUMA
LAZIMA utokwe machozi! Grace John mkazi wa Mzumbe, Mvomero mkoani Morogoro yupo kwenye wakati mgumu kutokana |
BADO ANAHITAJI MSAADA
“Madaktari wametupa moyo, wamesema watajaribu kumsaidia mwanangu.
Watamtoa hizo nyama ila kwa sababu kutabaki na mashimo lazima
wapandikize nyama nyingine.
“Tumeshakubaliana kuwa mimi ndiye nitakayekatwa sehemu ya nyama
kutoka kwenye makalio yangu kwa ajili ya kumsaidia mwanangu,” alisema
Bi. Grace, kilio kikisikika kwenye simu.
FAO kuzuia kutokea maafa ya chakula CAR
5:10 AM
No comments
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limetangaza kuwa, litachukua hatua za kuhakikisha kwamba, linazuia kutokea maafa ya chakula katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na mauaji yanayoendelea kufanywa na kundi la Kikristo la Anti-Balaka dhidi ya Waislamu.
Shirika hilo limeatangaza kuwa, linapanga kuanzisha mpango wa ustawi wa kilimo, kudhamini chakula kinachofaa kwa wote, kupambana na lishe duni na kuboresha chakula cha watu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na maeneo mengine duniani.
Tayari FAO imetiliana saini na serikali ya muda ya Bangui, mpango wenye thamani ya dola milioni nane. Wakati huo huo, mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yameendelea kutahadharisha kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati hususan Waislamu. Mamia ya Waislamu wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi yanayoendelea kufanywa na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
SOURCE: PRINCEMEDIA TZ BLOG
Saturday, March 22, 2014
WAPINZANI WAIPINGA HOTUBA YA RAIS KIKWETE
10:56 PM
No comments
Wenyeviti wa vyama vya upinzani nchini, kutoka kushoto ni James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF).
“Rais
tulitarajia angeongea kama mkuu wa nchi, lakini amezungumza kama
Mwenyekiti wa CCM na kutoa msimamo juu ya muundo wa Muungano jambo
ambalo hatukulitegemea,” alisema Mtatiro.Alisema kwa Rais kutoa msimamo
ni sawa na mwongozo jambo ambalo limevuruga mchakato mzima.Hofu ya
kuvunjika BungeWakizungumza nje ya Bunge, baadhi ya wajumbe wameeleza
kuwa hotuba ya Rais Kikwete kama ikitekelezwa uwezekano wa kupata Katiba
Mpya utakuwa mgumu.Mjumbe Luhaga Mpina alisema kwa jinsi rasimu
ilivyoandikiwa na kama muundo wa serikali mbili ukipita basi rasimu ya
Katiba itabidi iandikwe upya.“Rasimu yote imetengenezwa kwa mfumo wa
serikali tatu sasa hapa kuna hatari ya Bunge kukwama ,” alisema.Mtatiro
kwa upande wake alisema sasa kuna hofu ya kushindwa kupatikana Katiba
Mpya kwani Rais amewachanganya wajumbe na kama watapitisha maoni yake
itabidi rasimu kuandikwa upya.Mjumbe Mustapha Akoonay, alisema
upatikanaji wa katiba upo shakani kwani sasa upinzani utakuwa mkubwa juu
ya muundo wa muungano.“Kwa sasa nadhani itabidi turudi upya kwa
wananchi kupata kura ya maoni juu ya muundo wa muungano,” alisema.Lucy
Owenya alisema Rais amegeuza mkutano wa Bunge kuwa ni mkutano wa Chama
Cha Mapinduzi, kwani ameshindwa kabisa kutoa mwelekeo wa nchi na badala
yake ametoa msimamo wa CCM.“Kutokana na hili, naamini kabisa Bunge
halitakuwapo na ni bora iwe hivyo kwa kuwa amejibu hotuba ya Warioba na
kwa maana hiyo amepingana na mawazo ya wananchi.”Godbles Lema alisema
kuwa Rais hakuja kuhutubia taifa bali alikuja kufanya semina na kujibu
hotuba ya Warioba.Mjumbe huyo ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini
alionyesha shaka kuwa baada ya muda wa wiki tatu hakutakuwa na Bunge la
Katiba kwa kuwa wako baadhi ya watu ambao hawatakubali kilichofanywa na
Rais Kikwete.“Waliochukua fedha ni vyema wakaenda kumalizia nyumba zao
kwa kuwa kiongozi wetu amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwafurahisha
wanaCCM lakini kwa Watanzania hatutakubali,” alisema Lema.John Cheyo
alisema, “Mimi ninachokiona ni maridhiano tu, suala la kufumua rasimu
halinipi shida kwa kuwa vitu vyote vinavyoletwa bungeni huwa ni mali ya
Bunge na hivyo tutafanya tunavyoona sisi inafaa.”Mchungaji Peter Msigwa,
alisema kuwa kosa kubwa ambalo lilifanywa na upinzani ni kukubali na
kuruhusu Jaji Warioba atangulie kuwasilisha rasimu yake akasema hilo
ndilo lililowagharimu.Alitaka Bunge livunjwe mara moja ili warudi kwa
wananchi wakaamue na kuwahukumu kutokana na kile ambacho walikifanya
katika Bunge ambalo kwa maoni yake wamekula fedha za walipa kodi
bure.Naye Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa aliipongeza hutuba ya Rais
Jakaya Kikwete ya uzinduzi wa Bunge la Katiba.Lowassa ambaye pia ni
Mjumbe wa Bunge la Katiba, alisema kwa kifupi hotuba ya Rais Kikwete ni
nzuri. Lowassa alitoa kauli hiyo, wakati akitoka nje ya Bunge, muda
mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza hotuba ya uzinduzi wa Bunge
hilo.Naye Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Mchungaji Ernest Kadiva,
alisema hotuba ya Rais imetoa mwanga kwa wajumbe.“Rais ameonyesha
upungufu wa hoja mbalimbali hasa katika mfumo wa serikali tatu na sasa
ameacha kazi ya kuamua tuwe na mfumo wa serikali mbili au tatu ni ya
wajumbe,” alisema Mchungaji Kadiva.Hata hivyo, mjumbe mmoja ambaye
hakupenda kutaja jina lake alisema Rais alizungumza kama si mkuu wa nchi
bali Mwenyekiti wa CCM kwa sababu amesimamia hoja za chama
chake.Alisema hata kama mapendekezo ya Rais Kikwete yatatekelezwa, kamwe
hayatakuwa mwarobaini wa muungano. Mbunge wa Mwibara, Khangi Lugora
alisema hotuba hiyo waliitarajia na ndio maana kulikuwa na ubishi wa
nani atangulie kati ya Jaji Joseph Warioba na yeye kwa mujibu wa
kanuni.“Hotuba ilikuwa ikijaribu kumjibu Jaji Warioba na kwangu mimi
nilikuwa naona kuwa Rais naye alikuwa anachangia katika kuitunga Katiba
kwa kupitia hotuba yake hiyo. Tumeyasikia na sisi tutakwenda kutafakari
katika kutunga Katiba ambayo itakuwa ya Watanzania wote,” alisema.Kwa
upande wake Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Mkiwa Kimwanga, alisema
kilichofanyika ni Rais kwenda kutoa uamuzi juu ya mchakato uliokuwa
ufanywe na Bunge hilo.Kwa upande wake, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema
hakuitendea haki Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwamba Bunge hilo
haliwezi kutengeneza Katiba ambayo inalenga katika mfumo wa serikali la
mbili.“Itakuwa ni vigumu zaidi kupata Katiba Mpya, alikuwa anapinga
mambo ya msingi yaliyoelezwa katika rasimu ya kwanza. Hayo angeyaeleza
katika hatua ya awali ili rasimu hiyo ibadilishwe na si katika hatua hii
ya mwisho kabla ya kwenda kupigiwa kura na wananchi,” alisema.Alisema
ndani ya siku 70 haiwezekani kubadili rasimu hiyo ambayo imejikita
katika muundo wa serikali tatu kwenda katika muundo wa serikali
mbili.Ezekiah Olouch alitahadharisha wajumbe wenzake kutodharau maoni ya
wananchi waliyoyatoa katika rasimu hiyo ya pili.Alisema haiwezekani
tume zote ambazo zimeundwa kuangalia aina ya muundo wa serikali zije na
jibu moja kuwa namna ya kuimarisha muungano ni kuwapo kwa serikali
tatu.Jussa Ismail Ladu alisema kwa ufupi kwamba hotuba ya Rais Kikwete
imekuwa yenye sura ya CCM zaidi.Naye Mbunge wa Lulindi, Jerome Bwanausi,
aliielezea hotuba ya Rais kuwa imeibua mambo mengi ambayo baadhi ya
watu walikuwa wakiyaelewa tofauti, hivyo imeweka uelewa mzuri katika
baadhi ya maeneo.Profesa Costa Mahalu alisema ni hotuba ambayo
imewaachia changamoto, hasa katika eneo la muungano kwa sababu
wanahitajika kuunda muungano usiotetereka
PADRI AKUTA TUNGULI KABURINI KWA NGWEA
10:54 PM
No comments
Padri
wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Monica, Kihonda mkoani
Morogoro, Octavian Msimbe akionyesha tunguli zilizozungushiwa sanda
zilizokutwa kaburini kwa marehemu Ngwea.
PADRI
AKEMEAAwali, ilielezwa kuwa siku hiyo padri huyo alioteshwa ndoto usiku
juu ya uwepo wa vitu vya ajabu katika makaburi hayo ndipo akakemea kabla
ya kwenda kuvishuhudia asubuhi yake (Ijumaa iliyopita)
NA PRINCEMEDIA BLOG
Friday, March 21, 2014
Thursday, March 20, 2014
ANC:Rais Jacob Zuma hatajiuzulu ng'o
8:47 AM
No comments
Lakini amepuuzilia mbali wito wa Rais Zuma kuondolewa mamlakani kwa kura ya wabunge au hata kujizulu.
Hapo jana mdhibiti wa mali ya umma,Thuli Madonsela, alisema kuwa Zuma alitumia sehemu za pesa za umma zilizotengewa ukarabati wa nyumba yake kwa mambo yake binafsi.
Thuli Madonsela, aliamuru Rais Zuma kulipa pesa za ziada alizotumia za umma kukarabati nyumba yake ya kifahari, akisema kuwa alijinufaisha na pesa za umma kwa njia isiyofaa.
Ukarabati huo, ulijumuisha bwawa la kuogelea, kliniki binafsi na eneo la helikopta kuweza kutua.
Chama hicho kimesema kuwa ripoti hiyo imetolewa wakati usiofaa nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi Mei.
Simiyu yakabiliwa na Njaa kali!!!!!!!!!!!!!
2:19 AM
No comments
ZAIDI ya Watu lakini tano (500, 000) Mkoni
Simiyu, wanakabiliwa na Njaa kutokana na kutopata Mvua, hali inayofanya
Mazao yao kukauka kwa sababu ya jua.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti ametoa agizo hilo Machi 18, mwaka huu ambapo amewataka
Wananchi wa Mkoa huo, wasiuze Chakula kidogo walichopata kwani hivi
sasa hali ni mbaya huku akiwaagiza Viongozi wa Wilaya kuhakikisha kuwa
wanadhibiti uuzwaji wa Chakula kwa baadhi ya Wananchi wa maeneo husika.
Wakielezea hali ya Chakula katika Kata
zao, baadhi ya Madiwani wa Mkoa huo wamesema hali ya Chakula katika Kata
zao ni mbaya kutokana na Ukame unaosababishwa na hali ya mabadiliko ya
tabia ya Nchi.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa amewaagiza
Wananchi wa Mkoa huo, kulima Mazao yanayostahimili Ukame, kama Mtama,
Viazi Vitamu na Kunde ili kuendana na Hali ya Hewa.