Aliyekaa ni Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bi.Neema Ezekiel Mwaipela akifanya mahojiano na mwandishi wa habari A.J.T.C, Irene Lyimo
Mkufunzi wa Chuo cha Uandishi
wa habari na Utangazaji Arusha
Neema Ezekieli Mwaipela ameongea
na warembo wa chuoni hapo kuhusu urembo wa kujichubua kwani urembo huo una madhara makubwa sana na ni hatari kwa afya zao.
Hata hivyo amewaambia
warembo hao urembo wa kujichubua siyo urembo bali ni kuharibu sura na uhalisia wa ngozi zao, na ameendelea
kuwa elimisha kuhusu urembo huo wapo watu wengi wanaoona kwamba mtu mweupe ni
mtu mwenye hadhi kubwa ya kifedha ila sivyo wanavyofiri.
Mwaipela pia ameweza kuwapa warembo hao tofauti kati ya
urembo na uzuri “ ladies urembo una maanisha ni pale ushamaliza kuoga na
ukajipaka makorokoro na maanisha ukajifanyia make up, na Uzuri ni pale mtu
hajajipaka chochote kajipaka tuu mafuta usoni”.
Sanjari na hayo ameelezea athari za urembo wa kujichubua kuwa
zinaleta madhara makubwa sana na ni hatari kwa afya , athari hizo ni kama
kuharibu maumbile yao, kupoteza ngozi zao asilia,pamoja na kupata watoto ambao
hawapo vizuri kimaumbile.
Amehitimisha kwa kuwa shauri warembo hao kuwa wabaki na uzuri
“uhalisia” wao wa kuzaliwa na siyo watafute urembo ambao utakuja kuwasababishia
matatizo ha[po mbeleni hata kama siyo kwa sasa.
Na. IRENE LYMO.
0 comments:
Post a Comment