Watu wasiopungua 1,013 wameaga dunia kutokana na kuambukizwa virusi hivyo katika ukanda wa Afrika Magharibi.
Hatua hii ilichukuliwa huku Liberia ikitangaza kuwa ilihitaji kupata dawa la kufanyia majaribio liitwalo Zmapp baada ya kuiomba serikali ya Marekani.
Shirika la WHO lilisema kuwa lilikuwa limeombwa kupendekeza hatua hiyo kwa sababu ya kusambaa kwake na idadi kubwa ya vifo.
WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola
Shirika hilo lilisema kuwa mahali ambapo matibabu ya majaribio yanapofanyiwa panahitaji kuwa na ridhaa na matekeo ya jaribio hilo kukusanywa na kushiriki na wengine.
Katika ripoti iliyotolewa leo, shirika hilo linasema “Katika hali kama hizi za kuenea kwa ugonjwa huu, na iwapo masharti Fulani yataafikiwa, jopo hili limefikia makubaliano kuwa ni jambo la kimaadili kuingilia kati kwa mijarabu ambayo haijadhibitishwa huku ufanisi wake ukiwa haujulikani na adhari mbaya, kama matibabu au kinga.”
WHO ilitangaza kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kama janga la afya la dharura ulimwenguni.
Huku hayo yakijiri, serikari ya Liberia imesema kuwa madawa yatakayofanyiwa majaribio yatafikishwa nchini humo baadae juma hili – ingawa watengenezaji wa dawa madawa hayo Mapp Bio pharmaceutical walikuwa wameonya kuwa madawa hayo ni haba.
Zmapp imetumiwa kuwatibu wafanyikazi wawili wa US aid ambao walionyesha dalili ya kupata nafuu.
WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola nchini Liberia
Padri mmoja wa kanisa la Roman Catholic, aliyeambukizwa virusi vya Ebola nchini Liberia, na ambaye aliaga dunia baada ya kurejea nyumbani kwao nchuni Uhispania pia amedhaniwa kuwa alikuwa amepewa dawa hizo
0 comments:
Post a Comment