Tuesday, August 12, 2014

Wafanyabiashara ''utafiti dili!!''


kushoto ni Bwana Noel Taluka Akizungumza na mwanahabari.
Wafanyabiashara kote nchini  wameshauriwa   kujikita katika shughuli za kibiashara kwa kutafuta maeneo mazuri  ya kibiashara yatakayowasaidia kujipatia kipato ili kujikwamua kiuchumi badala ya kushinda vijiweni wakilaumu serikali.  


Hayo   yamesemwa    na  mmoja wa wafanyabiashara  Bwana   Noel   Taluka   ambaye   ni  muuzaji  wa  vifaa  vya  shule na muda wa matumizi ya wavuti  wakati akizungumza na wanahabari ofisi kwake Ndani  ya  chuo  cha  uandishi  wa  habari   na  utangazaji  jijini Arusha.

Bwana Taluka    amefafanua  kwamba    wafanyabiashara waliomakini ni lazima wafanye utafiti mahususi juu ya biashara wanayotaka kuifungua ili kuwafanya waendane sambamba na mahitajio ya jamii inayowazunguka.

Amebainisha kuwa mafanikio yakujihusisha na biashara ni makubwa endapo mfanyabiasha husika akifanya biashara kwa kuzingatia malengo yake na kujitahidi kuwa wabunifu katika biasharasha ili kuwavutia wateja wao.

Aidha bwana Taluka amesema suala la malalamiko ya wateja katika punguzo la bei ni moja ya changamoto ambayo inawakabilia wafanyabiasha wengi nchi lakini amesisitza kuwa biashara ni maelewano na hata siku moja hajawahi kushidwa kuelewana na wateja wake.


Amehitimisha       kwa    kuwashauri       wafanyabiashara       wengine        kuwa      na     tabia   ya     kufahamu      sehemu       ambazo      ni     rahisi      kufanyia   biashara     zao   pamoja     na   kuacha  tabia  Ya    kupandisha      bei      ya     bidhaa  hovyo.


Mwandishi 
Glory Kundi
www.lakenatron.blogspot.com














0 comments:

Post a Comment