NA MWANAIDI K OMARY
Samuel Eto'o akiwa na jezi ya timu yake ya Taifa.
Mshambuliaji mpya wa Everton raia wa
Cameroon Samuel Eto’o ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa tangu
aanze kuitumikia nchi yake mwaka 1995
ambapo Cameroon ilifungwa magoli 5 kwa 0 na Costa Rica.
Eto’o mwenye umri wa miaka 33
amestaafu akiwa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote kwa timu yake
ya taifa baada ya kupachika magoli 56 licha ya kutofunga goli lolote kwenye
fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo katika historia
yake amevichezea vilabu mbalimbali
barani Ulaya kama Real Madrid,Marlloca, Fc Barcelona,Inter Milan, Anzhi Makhachkala,Chelsea,na sasa anaichezea Everton akijiunga kwa uhamisho
huru nakupewa mkataba wa miaka miwili akitokea Chelsea.
Akizungumza uamuzi wake wa kustaafu
Eto’o ambaye ni kati ya wachezaji wa kiafrika waliowahi kukumbwa na maswahibu
ya kubaguliwa kutokana na rangi yake
barani Ulaya amewashukuru waafrika wote hususani masahabiki wake kwa
kuumuunga mkono na kumpenda.
Uamuzi wake ametangaza kupitia
matandao wa kijamii wa Instagram.
Michezo ya kimataifa aliyocheza tangu 1997-2014 kwenye timu ya taifa ya Cameroon.
Year
|
Apps
|
Goals
|
1997
|
3
|
0
|
1998
|
5
|
0
|
1999
|
1
|
0
|
2000
|
9
|
5
|
2001
|
9
|
2
|
2002
|
13
|
5
|
2003
|
7
|
2
|
2004
|
9
|
4
|
2005
|
6
|
1
|
2006
|
5
|
5
|
2007
|
3
|
1
|
2008
|
11
|
11
|
2009
|
8
|
5
|
2010
|
12
|
8
|
2011
|
9
|
4
|
2012
|
2
|
0
|
2013
|
4
|
2
|
2014
|
2
|
1
|
Total
|
117
|
56
|
0 comments:
Post a Comment