NICE MEDIA WORKS

KWA WAIMBAJI WA INJILI

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, August 30, 2014

AMISOM YASHAMBULIA KUSINI MWA SOMALIA.....


 
Maafisa wa jeshi la AMISOM

Maafisa wa serikali ya Somali wanasema kuwa vikosi vyao vikishirikiana na wanajeshi wa Amisom wameanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Alshabaab kusini mwa taifa hilo.

Lengo lao ni kuliteka jimbo la Lower Shabelle ambalo linajulikana kwa kuwa ngome kuu ya wapiganaji hao.

Gavana wa jimbo la Lower Shabelle Abdukadir Mohamed Nur amesema kuwa vikosi vya serikali vinapiga hatua kubwa katika oparesheni hiyo ilioanza siku ya ijumaa. NA ELIZABETH  NJAU.

Friday, August 29, 2014

TANZANIA NA BURUNDI ZAIMARISHA ALAMA ZA MIPAKA YAKE.....

Shughuli ya kuweka alama mpya ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi inaendelea, ambapo nchi hizo mbili jirani zinapima na kuweka mawe ya kimataifa kati ya mipaka. 
 Hafla rasmi ya zoezi hilo ilizinduliwa jana upande wa Tanzania katika kijiji cha Mugikomelo mpakani mwa nchi hizo mbili na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa nchi mbili. Katika hafla hiyo Rais Pierre Nkurunziza  wa Burundi amewashukuru Watanzania wote kwa mchango wao mkubwa katika kueleta amani na utulivu katika nchi yake, akisisitiza kuwa, licha ya nchi mbili hizo kuwa na mpaka lakini Tanzania inaruhusu maelfu ya wakimbizi wa Burundi kuingia nchini kwake bila kufuata taratibu za mipaka na uhamiaji, kwa sababu ya matatizo yanayowakabili  Warundi.
 Uwekaji mawe kwenye mpaka wa kimataifa kati ya nchi hizo mbili, unafanyika ikiwa ni baada ya kukamilika mchakato mrefu uliohusisha wataalamu wa nchi hizo wa kupima theluthi moja tu ya mpaka huo wa nchi mbili wenye kilometa 451.
Mpaka wa Tanzania na Burundi ni wa tano kwa urefu kati ya nchi 8 jirani na Tanzania, huku  Kenya ikiwa na mpaka mrefu zaidi wenye kilometa 769.


CHANZO: BBC
HABARI NA STEVEN  MULAKI

BAADA YA KUCHEZA MIAKA 17 MFULULIZO HATIMAYE ETO'O ASTAAFU KUCHEZEA TIMU YA TAIFA

ETO'O ASTAAFU KUICHEZEA TIMU YAKE YA TAIFA YA CAMEROON. 

NA MWANAIDI K OMARY


                                            Samuel Eto'o akiwa na jezi ya timu yake ya Taifa.

Mshambuliaji mpya wa Everton raia wa Cameroon Samuel Eto’o ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa tangu aanze kuitumikia nchi yake mwaka  1995 ambapo Cameroon ilifungwa magoli 5 kwa 0 na Costa Rica.
 
Eto’o mwenye umri wa miaka 33 amestaafu akiwa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote kwa timu yake ya taifa baada ya kupachika magoli 56 licha ya kutofunga goli lolote kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
 
Mshambuliaji huyo katika historia yake  amevichezea vilabu mbalimbali barani Ulaya kama Real Madrid,Marlloca, Fc Barcelona,Inter Milan, Anzhi Makhachkala,Chelsea,na sasa  anaichezea Everton akijiunga kwa uhamisho huru nakupewa mkataba wa miaka miwili akitokea Chelsea.
 
Akizungumza uamuzi wake wa kustaafu Eto’o ambaye ni kati ya wachezaji wa kiafrika waliowahi kukumbwa na maswahibu ya kubaguliwa kutokana na rangi yake  barani Ulaya amewashukuru waafrika wote hususani masahabiki wake kwa kuumuunga mkono na kumpenda.
Uamuzi wake ametangaza kupitia matandao wa kijamii wa Instagram.

Michezo ya kimataifa aliyocheza tangu 1997-2014 kwenye timu ya taifa ya Cameroon.

Year
Apps
Goals
1997
3
0
1998
5
0
1999
1
0
2000
9
5
2001
9
2
2002
13
5
2003
7
2
2004
9
4
2005
6
1
2006
5
5
2007
3
1
2008
11
11
2009
8
5
2010
12
8
2011
9
4
2012
2
0
2013
4
2
2014
2
1
Total
117
56

KWELI SHETANI AKIZEEKA ANAKUWA MALAIKA

ROONEY APEWA UNAHODHA WA ENGLAND. 

habari na YASINTA PETER



Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson  amemteua mshabuliaji wa Manchester United Wayne Rooney kuwa nahodha mpya  kuchukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na kiungo wa Liverpool Steven  Gerrard aliyestaafu mwezi uliopita.

Rooney mwenye umri wa miaka 28 ameshafunga magoli 40 kwenye timu ya taifa katika michezo 95 aliyocheza  hadi sasa na ataanza kuvaa kitamba cha unahodha kuanzia kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Uingereza na Norway septemba 3 mwaka huu.

Kocha  Roy Hodgson amesema anaamini Rooney anastahili kuwa nahodha wa Uingereza na kuteuliwa kwake kuwa nahodha wa Manchester United hivi karibuni kulidhihirisha kwamba anafaa kwa nafasi hiyo.

Aidha kocha huyo ametangaza kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki mwezi ujao dhidi ya Norway kabla ya kuikabili Uswis Septemba 8 mwaka huu.



Magoli kipa;Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), na Joe Hart (Manchester City) 

Walinzi ni Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Calum Chambers (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Danny Rose (Tottenham Hotspur),na  John Stones (Everton) 

Viungo ni Jack Colback (Newcastle United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal) Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), na Jack Wilshere (Arsenal) 

Washambuliaji ni  Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), na Danny Welbeck (Manchester United

UKISTAAJABU YA MUSSA .............................

KUNDI LA PANYA LAMUUA MTOTO KWA KUMTAFUNA

HABARI NA ELIZABETH SAID

Taarifa kutoka mjini Johannesburg Afrika Kusini zinasema - kuwa panya walimng'ata mtoto wa mwezi mmoja vidole na pua .

Mtoto huyo anasubiri kufanyia upasuaji wa kuumba maumbile yake ya usoni baada ya tukio hilo huko Alexandra, JohannesburgPanya walimvamia Erena Yekanyi nyumbani kwao katika kitongoji duni cha Alexandra. Wazazi wake wanasema kuwa hawana fedha za kumpeleka hospitalini kwa matibabu anayohitaji kwa haraka baada ya kunga'twa jumatatu.

“Nilikuwa nafua hapo nje naye Erena alikuwa ndani amelala.Mara nikamsikia akilia ndipo nikakimbia ndani kuangalia kulikoni nilimpata anavuja damu ''alisema mamake Thandaza. 
 
Sasa mtoto huyo anasubiri kufanyiwa upasuaji ambao utaumba upya pua lake na pia vidole vitatu vilivyong'atwa .

Mamake anasema madaktari katika hospitali ya Charlotte Maxeke AcademicHospital wanasubiri achangishe pesa za kutosha operesheni hiyo. Kulingana na ripoti hiyo tukio hilo sio la kwanza katika makazi hayo duni.

Inadaiwa kuwa watoto wengi na wazee wameripotiwa kung'atwa na panya hao wanaoonekana sio wa kawaida kutokana na kimo chao. Msemaji wa mji wa Johannesburg Nkosinathi Nkabinde panya ni wengi katika mitaa hiyo kutokana na hali duni ya usafi. Amesema kuwa kuna mipango ya kuangamiza wanyama hao.

Rubani mwanamke mkenya na mafanikio yake

Rubani wa kwanza wa kike nchini Kenya sasa amepata mafanikio zaidi kwa kufuzu kuwa rubani wa kwanza mwanamke barani Afrika kushika usukani wa ndege za kisasa aina ya Boeing 787 Dreamliner.

Imemchukuwa Rubani Irene Koki Mutungi kipindi cha zaidi ya miaka ishirini kufanikiwa kuvunja pingamizi zote zinazowazuia wanawake kuingia katika taaluma hiyo inayotawaliwa na wanaume.
Koki amefanya kazi ya urubani kwa kipindi cha miaka 20

MANJI ASISITIZA, SIMBA WAMEKURUPUKA KWA OKWI

Na Amalia seraphine

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema Simba wamekurupuka katika suala la Emmanuel Okwi.

Sunday, August 24, 2014

WAWILI WAFA KWA KWA EBOLA DRC

CHANZO BBC.  HABARI NA  GEORGE HILONGA
Picha ya Maktaba ikimwonyesha mgonjwa wa Congo mwenye umri wa miaka 43 akiwa kituo cha wagonjwa wa Ebola Septemba 29,2007
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imesema watu wawili wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola, uliolipuka kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.
Hao ni wagonjwa wa kwanza wa Ebola kuripotiwa nje ya Afrika Magharibi tangu kuzuka kwa ugonjwa huo huko, ingawaje haijaeleweka wazi kama vifo vya watu hao vinahusiana na mlipuko wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi.
Mpaka sasa watu 1,427 wamekufa kutokana na maambukizo ya virusi vya Ebola.
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema kasi na kiwango cha milipuko hiyo hakijawahi kutokea hapo kabla.
Watu wanaokadiriwa kufikia 2,615 Afrika Magharibi wameambukizwa ugonjwa wa Ebola tangu uzuke mwezi Machi mwaka huu.
Kirusi cha Ebola
Hakuna tiba inayojulikana kutibu ugonjwa huu lakini baadhi ya watu walioambukizwa virusi vya Ebola wamepata nafuu baada ya kupewa dawa ya Zmapp iliyo katika majaribio.
Hata hivyo dawa hiyo imeadimika kwa sasa.
Pia Jumapili, mfanyakazi wa afya wa Uingereza aliambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone na kurejeshwa Uingereza akisafirishwa na ndege ya jeshi la Uingereza, RAF.
Ni mgonjwa wa kwanza Mwingereza kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola wakati wa mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo.
Marekani imetuma vifaa vya tiba kusaidia kupambana na mlipuko wa Ebola nchini Liberia.
Watu kadha wamekufa katika kipindi cha mwezi uliopita baada ya kuugua homa isiyojulikana katika jimbo la Equateur katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Jumapili, Waziri wa Afya wa DR Congo Felix Kabange Numbi amesema watu wawili kati ya wanane waliopimwa ugonjwa Ebola wamethibitika kuambukizwa ugonjwa huo.
Ameiambia BBC kuwa eneo la karantini litawekwa katika eneo la kipenyo cha kilomita za mraba 100 katika eneo la Boende ambao wagonjwa wamegundulika.
Amesema huu ni mlipuko wa saba wa ugonjwa wa Ebola nchini DR Congo.
Virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa mara ya kwanza viligundulika nchini humo mwaka 1976 karibu na Mto Ebola.
Bwana Numbi amesema vipimo zaidi vinafanyika.
Kituo cha wagonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone moja ya nchi zilizoathirika kwa ugonjwa huo Afrika Magharibi
Jumamosi, bunge la Sierra Leone lilipitisha sheria mpya kuwa ni kosa la jinai kuwaficha wagonjwa wa Ebola.
Tayari watu zaidi wamekufa katika mlipuko huu wa Ebola kuliko milipuko mingine iliyowahi kutokea. Kama sheria hiyo itaidhinishwa na rais, wale wanaokamatwa kwa kuwaficha wagonjwa watakabiliwa na adhabu ya kifungo jela cha kufikia miaka miwili.
Hatua hii imekuja baada ya Ivory Coast kufunga mipaka yake ya nchi ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Nchi hiyo tayari imepiga marufuku safari za ndege kwenda na kutoka Sierra Leone, Liberia na Guinea.
Gabon, Senegal, Cameroon na Afrika Kusini zimechukua hatua kama hizo.
Shirika la Afya Duniani linasema upigaji marufuku safari za ndege hakusaidii, na kinachotakiwa ni madaktari zaidi na maafisa kusaidia kuwafuatilia walioambukizwa Ebola, ikiwa ni pamoja na kuwa na maabara zaidi za kuhama.
Wiki iliyopita, madaktari wawili wa Marekani waliruhusiwa kutoka hospitalini nchini Liberia baada ya kupewa dawa ya ZMapp drug, wakati ambapo madaktari watatu wa Liberia pia wanaendelea vema.
Ugonjwa wa Ebola unaenezwa kati ya binadamu kwa kugusana moja kwa moja na majimaji ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo. Ni moja kati ya magonjwa hatari kuliko yote duniani, ambapo asilimia 90 ya watu wanaoambukizwa ugonjwa wa Ebola hufariki dunia.

Saturday, August 23, 2014

MAGARI YA MSAADA YAREJEA URUSI


Malori ya misaada ya Urusi

Malori yote ya msafara wa misaada kutoka Urusi ambayo yalisafiri bila idhini hadi katika eneo linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa Ukraine siku ya ijumaa yamerudi nchini Urusi.
Afisa mmoja wa forodha amesema kuwa malori kadhaa yalikaguliwa na kurudi nchini Urusi.
Zaidi ya malori mia mbili ya misaada yalisafiri hadi katika mji wa Luhansk siku ya ijumaa,baada ya Urusi kusema kuwa imechoka kungojea idhini kutoka kwa serikali ya Ukraine.
Urusi inasema kuwa msaada huo ulikuwa wa kibinaadamu,lakini mataifa ya Magharibi yanasema kuwa unatumiwa na Urusi kuvamia Ukraine.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kufanya mazungumzo mjini Kiev na rais wa Ukraine Petro Poroshenko pamoja na waziri mkuu Arseniy Yatsenyuk. CHANZO BBC........HABARI NA ELIZABETH NJAU

Thursday, August 21, 2014

ANGALIA WANAFUNZI WA AJTC WAKIWA KATIKA MAZOEZI YA VITENDO

Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha AJTC wakisikiliza moja ya presentation zilizokwa zikitolewa na wanafunzi wenzao hii ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo



 Mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho Bahati Mshana akiwasilisha mada yake mbele ya wanafunzi

 somo la  Public raations likiwa linawasilishwa kwa vitendo na baadhi ya wanafunzi chuoni hapo 

Wednesday, August 13, 2014

habari za kimataifa ::Liberia kutumia 'Zmapp' kutibu Ebola

WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola nchini Liberia
Jopo la wataalam wa shirika la afya duniani WHO limeamua kwamba watu wanaweza kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa katika mwili wa binaadamu kutibu ugonjwa wa ebola,iwapo maagizo fulani yataheshimiwa ikiwemo ruhusa ya mgonjwa.

Tuesday, August 12, 2014

Wafanya biashara wa soko la kwa morombo mkoani Arusha wameimba serikali kuboresha miundo mbinu



Wafanya biashara wa soko la kwa morombo mkoani Arusha wameimba serikali kuboresha miundo mbinu ndani ya soko hilo

Liberia kupatiwa dawa ya majaribio ya Ebola

Ebola Krankenhaus Liberia

Liberia imetangaza kuwa hivi karibuni itapokea dozi za dawa za majaribio ya kutibu ugonjwa wa Ebola kutoka Marekani, ambazo itazitumia kwa madaktari wawili walioambukizwa virusi hivyo.

Serikali ya Marekani ilithibitisha kuwa iliwaunganisha maafisa wa Liberia na kampuni inayotengeneza dawa hiyo iitwayo ZMapp. Katika taarifa yake, kampuni hiyo ya Mapp Biopharmarceutical yenye makao yake jimboni California, ilisema kuwa katika kujibu maombi kutoka kwa taifa la Afrika magharibi ambalo halikutajwa, ilikuwa imeishiwa na ugavi wa dawa hiyo.

Misaada ya Urusi yaelekea Ukraine

Russischer Hilfskonvoi für die Ukraine 12.08.2014

Watoa misaada ya kibinaadamu, wakiwa na shehena ya misaada hiyo kutoka Urusi leo hii limeelekea nchini Ukraine. Likiwa nchini Ukraine kundi hilo litasindikizwa na wawakilishi wa asasi ya usalama na ushirikiano ya Ulaya.

Mkuu wa polisi auawa nchini Libya


Kanali Muhammad Suwaysi aliteuliwa kama mkuu wa polisi mjini Tripoli mwaka 2012


Mkuu wa polisi katika mji mkuu wa Libya Tripoli, ameuawa na watu wasiojulikana.
Kanali Muhammad Suwaysi alipigwa risasi, alipokuwa anaondoka kwenye mkutano katika eneo la Tajoura , mtaa ulio mashariki mwa mji mkuu Tripoli.

Wenzake wawili walitekwa nyara kwa mujibu wa taarifa za wizara ya ndani.

Libya imekumbwa na vurugu zinazosemekana kusababishwa na wapiganaji wa kiisilamu, ambao walisababisha harakati za kumuondoa mamlakani Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Maelfu ya watu wamelazimika kutoroka Tripoli.

Zaidi ya miaka mitatu baada ya kuondolewa mamlakani kwa Gadaffi, jeshi la polisi nchini Libya linasemekana kuwa dhaifu,
ikilinganishwa na wapiganaji wanaodhibiti sehemu kubwa za nchi hiyo



Wapiganaji wa kiisilamu ambao wamekuwa wakizua vurugu nchini Libya
Afisa huyo aliuawa wakati alipokuwa anatoka katika mkutano na maafisa wa mtaa wa Tajoura.
Maafisa wengine wawili waliokuwa naye, walitii masharti ya washambuliaji na kuondoka kwenye gari lao huku wakitekwa nyara.
Mamia ya watu wamefariki katika miezi ya Julai na Agosti katika kile kinachoonekana kuwa kukithiri kwa vurugu.

Habari Na.IRENE LYMO.

Warembo watakiwa kuwa makini na vipodozi wanavyotumia



 Aliyekaa ni Mkufunzi wa chuo cha  uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bi.Neema Ezekiel Mwaipela akifanya mahojiano na mwandishi wa habari A.J.T.C, Irene Lyimo

Mkufunzi wa Chuo cha Uandishi  wa habari na Utangazaji Arusha  Neema Ezekieli Mwaipela  ameongea na warembo wa chuoni hapo kuhusu urembo wa kujichubua kwani  urembo huo una madhara makubwa sana  na ni hatari kwa afya zao.

Hata hivyo amewaambia  warembo hao urembo wa kujichubua siyo urembo bali ni kuharibu sura  na uhalisia wa ngozi zao, na ameendelea kuwa  elimisha kuhusu urembo huo  wapo watu wengi wanaoona kwamba mtu mweupe ni mtu mwenye hadhi kubwa ya kifedha ila sivyo wanavyofiri.

Mwaipela pia ameweza kuwapa warembo hao tofauti kati ya urembo na uzuri “ ladies urembo una maanisha ni pale ushamaliza kuoga na ukajipaka makorokoro na maanisha ukajifanyia make up, na Uzuri ni pale mtu hajajipaka chochote kajipaka tuu mafuta usoni”.

Sanjari na hayo ameelezea athari za urembo wa kujichubua kuwa zinaleta madhara makubwa sana na ni hatari kwa afya , athari hizo ni kama kuharibu maumbile yao, kupoteza ngozi zao asilia,pamoja na kupata watoto ambao hawapo vizuri kimaumbile. 

Amehitimisha kwa kuwa shauri warembo hao kuwa wabaki na uzuri “uhalisia” wao wa kuzaliwa na siyo watafute urembo ambao utakuja kuwasababishia matatizo ha[po mbeleni hata kama siyo kwa sasa.

 Na. IRENE LYMO.

Mtuhumiwa azua kihoja mahakamani Rwanda



Rwanda imekuwa ikiendedesha harakati za upatanishi na pia kuwakumbuka waliokufa katika mauaji hayo

Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Emmanuel Mbarushimana amekataa uendeshwaji wa kesi yake na mahakama ya Kigali kwa kutoa pingamizi kwamba hana haki zilizo sawa na mwendesha mashitaka.
Mshukiwa huyo alikabidhiwa Rwanda na nchi ya Denmark mapema mwezi wa saba mwaka huu ili kujibu mashitaka ya kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Mushukiwa huyo Bwana Emmanuel Mbarushimana amesema kesi yake haiwezi kusikizwa hadi pale atakapopata haki zilizo sawa na mwendesha mashitaka.

Liberia kutumia 'Zmapp' kutibu Ebola

WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola nchini Liberia

Jopo la wataalam wa shirika la afya duniani WHO limeamua kwamba watu wanaweza kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa katika mwili wa binaadamu kutibu ugonjwa wa ebola,iwapo maagizo fulani yataheshimiwa ikiwemo ruhusa ya mgonjwa.

Tangazo hilo linajiri huku shirika hilo likitangaza kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo imepita watu 1000 na kwamba kasisi wa uhispania aliyeondolewa nyumbani mwake baada ya kuambukizwa ugonjwa huo amefariki.

AJTC yaja na wazo kufungua TV

Kushoto ni Bwana Kitomari akizungumza na mwanahabari
Mkuu wa kituo cha runinga katika chuo cha uandishi wa habari  na utangazaji arusha ajtc bwana Godlisten kitomari amesema mwitikio wa wanafunzi unazidi kuwa mkubwa huku wakifanya vizuri.
Bwana kitomari amesema wanafunzi kwa sasa wanajitahidi kufanya vipindi kama runinga kubwa nyingine nchini.
Pamoja na wanafunzi kufanya vizuri lakini pia ametaja kuwa  wanafunzi wanafanya ushindani wa vipindi kwa madarasa huku wakifuatilia kwa ukaribu mifumo ya vipindi katika runinga nyinginezo kubwa ndani na nje ya nchi.

Wafanyabiashara ''utafiti dili!!''


kushoto ni Bwana Noel Taluka Akizungumza na mwanahabari.
Wafanyabiashara kote nchini  wameshauriwa   kujikita katika shughuli za kibiashara kwa kutafuta maeneo mazuri  ya kibiashara yatakayowasaidia kujipatia kipato ili kujikwamua kiuchumi badala ya kushinda vijiweni wakilaumu serikali.  


Hayo   yamesemwa    na  mmoja wa wafanyabiashara  Bwana   Noel   Taluka   ambaye   ni  muuzaji  wa  vifaa  vya  shule na muda wa matumizi ya wavuti  wakati akizungumza na wanahabari ofisi kwake Ndani  ya  chuo  cha  uandishi  wa  habari   na  utangazaji  jijini Arusha.

Bwana Taluka    amefafanua  kwamba    wafanyabiashara waliomakini ni lazima wafanye utafiti mahususi juu ya biashara wanayotaka kuifungua ili kuwafanya waendane sambamba na mahitajio ya jamii inayowazunguka.

Liberia kutumia 'Zmapp' kutibu Ebola

Liberia kutumia 'Zmapp' kutibu Ebola

 

WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola nchini Liberia
Jopo la wataalam wa shirika la afya duniani WHO limeamua kwamba watu wanaweza kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa katika mwili wa binaadamu kutibu ugonjwa wa ebola,iwapo maagizo fulani yataheshimiwa ikiwemo ruhusa ya mgonjwa.

Tangazo hilo linajiri huku shirika hilo likitangaza kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo imepita watu 1000 na kwamba kasisi wa uhispania aliyeondolewa nyumbani mwake baada ya kuambukizwa ugonjwa huo amefariki.


Kuidhinisha utumizi wa dawa ilio katika majaribio ni swala gumu.

Dawa hiyo ambayo haijajaribiwa imetumiwa na raia wawili wa kutoa msaada kutoka marekani ambao afya yao imeimarika,lakini kasisi huyo wa Uhispania ambaye pia aliitumia dawa hiyo ameaga dunia.

Watu wasiopungua 1,013 wameaga dunia kutokana na kuambukizwa virusi hivyo katika ukanda wa Afrika Magharibi.



Hatua hii ilichukuliwa huku Liberia ikitangaza kuwa ilihitaji kupata dawa la kufanyia majaribio liitwalo Zmapp baada ya kuiomba serikali ya Marekani.

Shirika la WHO lilisema kuwa lilikuwa limeombwa kupendekeza hatua hiyo kwa sababu ya kusambaa kwake na idadi kubwa ya vifo.




WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola
Shirika hilo lilisema kuwa mahali ambapo matibabu ya majaribio yanapofanyiwa panahitaji kuwa na ridhaa na matekeo ya jaribio hilo kukusanywa na kushiriki na wengine.



Katika ripoti iliyotolewa leo, shirika hilo linasema “Katika hali kama hizi za kuenea kwa ugonjwa huu, na iwapo masharti Fulani yataafikiwa, jopo hili limefikia makubaliano kuwa ni jambo la kimaadili kuingilia kati kwa mijarabu ambayo haijadhibitishwa huku ufanisi wake ukiwa haujulikani na adhari mbaya, kama matibabu au kinga.”



WHO ilitangaza kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kama janga la afya la dharura ulimwenguni.

Huku hayo yakijiri, serikari ya Liberia imesema kuwa madawa yatakayofanyiwa majaribio yatafikishwa nchini humo baadae juma hili – ingawa watengenezaji wa dawa madawa hayo Mapp Bio pharmaceutical walikuwa wameonya kuwa madawa hayo ni haba.



Zmapp imetumiwa kuwatibu wafanyikazi wawili wa US aid ambao walionyesha dalili ya kupata nafuu.




WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola nchini Liberia
Padri mmoja wa kanisa la Roman Catholic, aliyeambukizwa virusi vya Ebola nchini Liberia, na ambaye aliaga dunia baada ya kurejea nyumbani kwao nchuni Uhispania pia amedhaniwa kuwa alikuwa amepewa dawa hizo.



Hata hivyo, dawa hizo zimejaribiwa kwa nyani tu na bado haijatathminiwa kuwa ni salama kwa binadamu.

Shirika la afya dunini WHO linasema kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Africa sasa imepita watu 1000.



Hii leo wataalam hao wa WHO wamekubaliana kwamba utumizi wa dawa hizo utakubalika iwapo kutakuwa na uwazi huku rukhsa ikitolewa na wote wanaoshiriki katika tiba hiyo mbali na kuficha siri ya mgonjwa aliyetibiwa.



Na huku hayo yakijiri Liberia ambalo ndio taifa lililoathiriwa sana na ugonjwa huo lilianza kutumia dawa hizo kutoka marekani kabla ya uamuzi wa utumizi wake kutolewa na WHO. 



      by MARTINI SAIGILU

Tuesday, August 5, 2014

Baada ya kupigwa na binti wa Obama, haya ndiyo majibu aliyo toa msichana huyo nakushangaza watu


Binti wa Raisi wa Marekani, Malia Obama mwenye umri wa miaka 16 alimpiga/alimgonga kwa bahati mbaya msichana aliyefahamika kwa jina la Bridget Truskey walipokuwa katika tamasha kubwa la muziki la Lollapalooza nchini Marekani.