Saturday, November 2, 2013

FUATILIA RATIBA YA LIGI KUU YA UINGEREZA LEO JUMAMOSI, HUKU LEWANDOSKI AKITUMA SALAMU KWA ARSENAL!!


APIGA HETITRIKI, DORTMUND YAIBONDA STUTTGART  6-1!
Robert Lewandowski amepiga Bao 3 wakati Borussia Dortmund ilipotoka nyuma na kuibamizaLEWANDOWSKI-SHUJAAStuttgart Bao 6-1 na kutua kileleni mwa Bundesliga.
Karim Haggui aliifungia Stuttgart Bao lao mapema lakini Sokratis Papastathopoulos akasawazisha kwa kichwa na Marco Reus kufunga Bao la pili kwa Dortmund.
Ndipo zikaja Bao 3 za Lewandowski na Pierre-Emerick Aubameyang kumalizia Bao la 6.

Tayari Msimu huu Lewandowski amepiga Bao 12 katika Mechi 14 na kuifanya Dortmund iongoze Bundesliga ikiwa Pointi 2 mbele ya Bayern Munich ambao wana Mechi moja mkononi na wanacheza Ugenini na Hoffenheim Siku ya Jumamosi.
Dortmund sasa wanaingoja Arsenal itembelee Signal Iduna Park hapo Jumatano kwa Mechi ya Marudiano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Katika Mechi ya Kwanza ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa Mwezi Oktoba, Arsenal, wakiwa kwao Emirates, walilala Bao 2-1 na Borussia Dortmund.fixtures-2013-14-premier-league_3ac9d.png
Untitled_picture_9677d.jpg
POSTED BY:Emanuel Onesmo Ndanshau

0 comments:

Post a Comment