Monday, November 4, 2013

MKANGANYIKO WAIBUKA KUHUSIANA NA MALIPO YA ADA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA


Wanafunzi wa Uandishi wa Habari na Utangazaji ngazi ya Stashahada wakiwa mbele ya jengo la utawala na Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo hicho.

Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha, AJTC. Wamezua gumzo baada ya kuchanganywa na malipo ya mtaala Mpya unaotumika vyuoni kwa sasa.

Akizungumzia mkanganyiko huo Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuoni hapo Bw. GEORGE SILANGE, amesema kuwa anachanganywa na malipo ya ada haswa kwa wanafunzi wanaotumia mtaala mpya kwani wamekua wakirudishwa ada mara kwa mara, kutokana na mpangilio usio rasmi vyuoni

Aidha Rais huyo ameuomba uongozi wa chuo kufuatilia kwa umakini malipo hayo kwani yatakua yanapotosha wanafunzi wengi na kujikuta wakishindwa kuelewana na wazazi wao kwani wazazi hawatakuwa tayari kulipa ada kama ilivyopangwa na uongozi wa chuo hicho

Kumekuwepo ha hali ya sintofahamu kwa wanafunzi kutokana na malalamiko mbalimbali yakiwepo ya Darasa la Udzungwa na Manyara kupatiwa barua yakwenda likizo ya wiki mbili nyumbani huku wakiagizwa kurudi na hala ya mhula mwingine wakati ndiyo kwanza wamemaliza miezi mitatu ya mwanzo bado hawajamaliza Muhula wa kwanza.

Mmoja wa wanafunzi wa darasa la Udzungwa aliyejitambulisha kwa jina la AGAPE MSUMARI alielezea kushtushwa kwake na yaliyoandikwa kwenye barua,

"nashindwa kuelewa malipo ya chuo hiki yanaendaje ndg mwandishi kwasababu nimemaliza miezi mitatu tuu leo hii naambiwa nikirudi likizo nije na ada ya muhula mwingine hivi kweli wazazi watanielewa?" alisema.

Nae mkufunzi wa taaluma katika chuo hicho Bw.Adson Kagie Mayagila amesema kuwa utararatibu wa malipo ya ADA unafanyika kila mwishoni mwa muhula na wala siyo vinginevyo,

"Kama barua zimeonyesha kuwa darasa la Udzungwa na Manyara wanatakiwa kurudi na ada ya muhula ni makosa tuu yakiuandishi yametokea kwani kwa kawaida malipo ya ada yanafanyika kila mwisho wa muhula"alisema.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment