Thursday, October 31, 2013

SIMBA YAMWAGA POINTI, SARE NA KAGERA, MASHABIKI VURUGU TUPU!!

PENATI DAKIKA ZA MAJERUHI YAWAKATA MAINI SIMBA!!!

ALHAMISI: JKT RUVU v YANGA, JE YANGA KUKWAA KILELENI?
VPL_2013-14_LOGO-NEWLEO Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam uligeuka vurugu tupu mara baada ya Kagera Sugar kusawazisha Bao kwa Penati katika Dakika za Majeruhi na Mashabiki kung’oa Viti na kuvitupa Uwanjani hali ambayo iliwalazimu Polisi kufyatua Mabomu ya Machozi.

Mechi hiyo ilimalizika kwa Bao 1-1 na kuiacha Simba ikibaki Nafasi ya 4 huku Kagera Sugar ikipanda nafasi moja.
Simba ndio waliotangulia kupata Bao katika Dakika ya 45 ambalo llifungwa na Mchezaji toka Burundi, Amisi Tambwe, alieinasa pasi ya Betram Mombeki na kuwatambuka Mabeki Salum Kanoni na Ernest Mwalupani na kisha kufunga.
Huku Simba wakitegemea ushindi kwani Bango la Dakika za Nyongeza lilikuwa limeshaanikwa na Refa wa Akiba likionyesha Dakika 4 na nusu ya Dakika hizo kuyoyoma, Beki wa Simba Joseph Owino akamwangusha Daudi Jumanne ndani ya Boksi na Refa kutoa Penati iliyofungwa na Salum Kanoni.
Alhamisi Jioni kwenye Uwanja wa Taifa JKT Ruvu watapambana na Mabingwa Watetezi Yanga kwenye Mechi pekee ya Ligi Kuu Vodacom ambapo ushindi kwa Yanga utawafanya wakamate usukani wa Ligi.
VIKOSI
Simba: Abuu Hashimu, Nassoro Masoud 'Chollo', Issa Rashid, Joseph Owino, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Said Ndemla, Betram Mwombeki, Amisi Tambwe , William Lucian
Kagera Sugar: Agaton Antony, Salum Kanoni, Martin Muganyizi, Ernest Mwalupani, Malegezi Mwangwa, Zuberi Dabi, Benjamin Asukule, George Kavilla, Themi Felix, Daudi Jumanne, Paul Ngwai 
RATIBA:
Ijumaa Novemba 1
JKT Ruvu vs Yanga
Jumamosi Novemba 2
Mgambo Shooting vs Coastal Union
Tanzania Prisons vs Oljoro JKT
Azam vs Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar vs Rhino Rangers
Jumapili Novemba 3
Mbeya City vs Ashanti United
Jumatano Novemba 6
JKT Ruvu vs Coastal Union
Ashanti United vs Simba
Kagera Sugar vs Mgambo Shooting
Rhino Rangers vs Tanzania Prisons
Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar
Alhamisi Novemba 7
Azam vs Mbeya City
Yanga v JKT Oljoro
MSIMAMO-LIGI KUU VODACOM 
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Azam FC
11
6
5
0
17
7
10
23
2
Mbeya City
11
6
5
0
16
8
8
23
3
Young Africans
11
6
4
1
24
11
13
22
4
Simba SC
12
5
6
1
22
11
11
21
5
Kagera Sugar
12
4
5
3
13
10
3
17
6
Ruvu Shootings
11
4
4
3
13
10
3
16
7
Mtibwa Sugar
11
4
4
3
16
15
1
16
8
Coastal Union
11
3
6
2
10
6
4
15
9
JKT Ruvu
11
4
0
7
9
12
-3
12
10
Rhino Rangers
11
2
4
5
9
15
-6
10
11
Ashanti United
11
2
4
5
10
19
-9
10
12
Tanzania Prisons
11
1
5
5
6
15
-9
8
13
JKT Oljoro
11
1
4
6
8
16
-8
7
14
Mgambo JKT
11
1
2
8
3
21
-18
5

POSTED BY:Emanuel Onesmo Ndanshau

0 comments:

Post a Comment