Wednesday, November 13, 2013

WANAHABARI WAHASWA KUEPUKA UKIMWI.

KIONGOZI WA DARASA LA SELOUS  BW. KYIAN AKITOA MAELEKEZO KUHUSU JINSI UGONJWA WA UKIMWI UNAVYO ENEA

WANDISHI WA HABARI  WAMETAKIWA KUANDAA  VIPINDI VYA KUELIMISHA  JAMII VINAVYO HUSIANA NA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI IKIWA NI MOJA YA KAZI ZAO

KAULI HIYO IMETOLEWA JANA NA WANAFUNZI WA DARASA LA SELUU WAKATI WAKIWASILISHA SOMO LA JINSIA AMBALO LINAUSIANA NA VVU/UKIMWI ILIYOTOLEWA KATIKA UKUMBI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI(AJTC)MKOANI ARUSHA.

AKIWASILISHA MADA HIYO BW KYIAN TOROGE ALIELEZEA NAMNA UGONJWA HUO UNAVYO ENEZWA KUWA NI PAMOJA NA KUCHANGIA VITU VYENYE NCHA KALI KAMA VILE NYEMBE, SINDANO PAMOJA NA NGONO ZEMBE.

AIDHA BWANA TOROGE ALISEMA KUWEPO KWA SOMO HILI KUNAMSAIDIA MWANDISHI WA HABARI KUWEZA KUANDIKA HABARI ZA KUELIMISHA JAMII JINSI YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

HATA HIVYO KATIKA UWASILISHAJI  WA SOMO HILO WANAFUNZI WALIONYESHA HAMASA YA KUENDELEA NA SOMO HILO WALISEMA MFUMO WA DIGITAL UMESAIDIA KUWEPO KWA SOMO HILO JIPYA LA USAWA WA KIJINSIA  LENYE KUELIMISHA.


MMOJA WA WANAFUNZI (BW  DENNIS  KAZENZELE) ALIYESIMAMA  WA CHUO CHA UANDISHI WA  HABARI NA UTANGAZAJI   AKIULIZA SWALI .




RAIS WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA BW.GEORGE SILANGE AKITOA MAELEZO JINSI YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI.

BI.BAHATI MSHANA AKIELEZEA VITU VINAVYOWEZA KUCHANGIA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA UKIMWI.

KATIBU WA SERIKALI YA WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA BW.IZACK MWACHA  AKICHANGIA MADA YA NAMNA YA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA UKIMWI.




PICHANI JUU NI WANAFUNZI WA DARASA LA SELOU WAKIWASILISHA MADA MBALIMBALI JUU YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA UKIMWI.

POSTED BY:Mwajuma Abdul.
Edited By:Mariam Hassan na Virginia Chidiaka.
Photo by:Emanueli Ndanshau na Khadija Omary.

0 comments:

Post a Comment