Saturday, November 9, 2013

NIYONZIMA ACHUKUA TUZO TATU TUZO ZA MWANASPOTI 2013 USIKU WA JANA, KASEJA ,KIEMBA ,SAMATA NAO WANG'ARA.

Haruna na tuzo zake tatu
KIUNGO wa Yanga SC, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima raia wa Rwanda, ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa gazeti la Mwanaspoti, akiwashinda Amri Kiemba, Shomary Kapombe wa Simba SC na Themi Felix wa Kagera Sugar. Katika hafla iliyofana kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wachezaji wengi, mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa (TEKNOHAMA) Januari Makamba, mchezaji Niyonzima aliondoka na tuzo tatu, nyingine ya mchezaji wa kigeni na 11 Bora wa Mwanaspti.
Haruna akipokea tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Kigeni kutoka kwa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA)  

Katika tuzo ya mchezaji bora wa kigeni, Niyonzima aliwashinda mchezaji mwenzake wa Yanga, mshambuliaji wa Kiganda, Hamisi Friday Kiiza na mshambuliaji wa Azam kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche. Mchezaji wa Azam FC, Joseph Kimwaga aliwashinda Juma Luizio wa Mtibwa Sugar na Ramadhani Singano ‘Messi’ katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mchezaji Chipukizi. Mwanahamisi Omar wa Mburahati Queens aliwashinda Shelida Boniface na Fatuma Mussa katika ya Mchezaji Bora wa kike, wakati Mbwana Samatta aliwashinda Henry Joseph aliyekuwa anacheza Kongsvinger ya Norway kabla ya kurejea Simba SC msimu huu na mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu katika tuzo ya mwanasoka anayecheza nje. 
Haruna akipokea hundi ya Sh. Milioni 5 kutoka kwa Naibu Waziri wa TEKNOHAMA, Januari Makamba. Wengine kulia ni Zuhura Muro, Mwenyekiti wa Bodi wa MCL na Tido Mhando kushoto, Ofisa Mtendaji Mkuu wa MCL
 Oden Mbaga aliwashinda Martin Sanya na Ibrahim Kidiwa katika tuzo ya Refa bora, wakati Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ aliwashinda Muingereza Stewart Hall wa Azam na Mholanzi Ernie Brandts wa Yanga katika tuzo ya kocha bora. Thomas Ulimwengu alishinda tuzo ya bao bora alilofunga katika mechi dhidi ya Ivory Coast kuwania tiketi ya Kombe la Dunia, wakati Kipre Tchetche ameshinda tuzo ya Mfungaji bora. Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, David Mwantika, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, Haruna Niyonzima, Themi Felix, Mbwana Samatta na Kipre Tchetche wameteuliwa katika ’11 Bora’ wa Mwanaspoti. Zilizotolewa pia tuzo za heshima kwa wachezaji wa zamani nchini akina Nicholas Akwitende, John Lyimo, Mbwana Abushiri, Omar Zimbwe, Jellah Mtagwa na mtangazaji wa zamani maarufu, Mshindo Mkeyenge. Mkeyenge aliyeanza kutangza tangu miaka ya 1960 Radio Tanzania (RTD) aliwahuzunisha wengi baada ya kuwasili jukwaani akiwa amebebwa kutokana na kukatwa mguu kwa sababu ya maradhi ya kupooza. Hadhara Charles alipewa tuzo ya kipaji maalum, wakati Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga alipewa tuzo ya Utawala Bora katika soka. Washindi walipewa na zawadi za fedha, Niyonzima Sh. Milioni 5, wengine Sh. Milioni 1 na wengine 500,000. Kwa ujumla tuzo hizo zilizosindikizwa na burudani ya wanamuziki Juma Nature, Joh Makini na King Kiki zilifana.
HAFLA YA TUZO ZA WANASOKA BORA TANZANIA WA GAZETI LA MWANASPOTI ILIVYOFANA JANA MLIMANI FUATILIA HAFLA YA TUZO ZA WANASOKA BORA TANZANIA WA GAZETI LA MWANASPOTI ILIVYOFANA JANA MLIMANI CITY HAPA!!.

Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga kushoto akimkabidhi tuzo ya Ufungaji Bora mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast katika tuzo za gazeti la Mwanaspoti usiku wa jana ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. 


Naibu Waziri wa TEKNOHAMA, Januari Makamba kushoto akimkabidhi tuzo ya Mwanasoka Bora, kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima kulia. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya MCL, Zuhura Muro


Rais wa heshima wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Said El Maamry akimkabidhi tuzo ya Mchezaji bora wa Tanzania anayecheza nje, mwakilishi wa mshindi wa tuzo hiyo, Mbwana Samatta wa TP Mazembe ya DRC.


Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Geoffrey Nyange 'Kaburu' akimkadhi tuzo Refa Bora, Oden Mbaga


Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Zamoyoni Mogella akimkabidhi tuzo ya bao bora, mwakilishi wa mshindi wa tuzo hiyo, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC


Kipa mpya wa Yanga SC, akipokea Tuzo ya 11 Bora kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya MCL, Zuhura Muro kushoto


Amri Kiemba wa Simba SC akipokea tuzo ya 11 Bora


Winga wa Azam FC, Joseph Kimwaga akipokea tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi kutoka kwa Mohammed Rweyemamu, Mjumbe wa Bodi ya MCL 


Mwanahaisi Omar akipokea tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike kutoka kwa Makamu Rais wa Shirikisho la Soka la Wanawake (TWFA), Rose Kisiwa kushoto


Makamba akimkabidhi tuzo ya heshima, Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Nicholaus Akwitende kulia 


Nahodha mwingine wa zamani wa Taifa Stars, John Lyimo akipokea tuzo ya heshima kulia


Nahodha mwingine wa zamani wa Taifa Stars, Mbwana Abushiri akipokea tuzo yake


Nahodha mwingine wa zamani Taifa Stars, Omar Zimbwe akipokea tuzo yake ya heshima


Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars, Said George aimpokelea tuzo Jellah Mtagwa


Mtangazaji maarufu wa mpira wa zamani wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), sasa TBC, Mzee Mshindo Mkeyenge (katikati) akipokea tuzo yake ya heshima


Meneja Uhusiano wa Vodacom, Salum Mwalimu akimkabidhi Tenga tuzo ya Utawala Bora


Wachezaji na wawakilishi wa wachezaji walioteuliwa katika 11 Bora ya gazeti la Mwanaspoti wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushinda tuzo zao


Mzee King Kiki alitumbuiza 


Rapa Joh Makini akitumbuiaza


Rapa Joh Makini akiwataka waalikwa wainue mikono juu


Na kweli watu wazima waliiua mikono kucheza Hip hop


Rapa Juma Nature akitumbuiza


Ofisa wa Azam FC, Patrick Kahemele akipokea tuzo ya 11 Bora kwa niaba ya Kipre Tchetche


Juma Kaseja na Amri Kiemba baada ya kupokea tuzo zao


Msanii akionyesha utundu na kipaji cha kunyumbulika


Hivi ni vipaji adimu


TBC1 walikuwa live jana


Amerudi Yanga huyu; Kipa wa Coastal Union, Shaaban Kado kushoto akifurahia jambo na kipa mpya wa Yanga SC, Juma Kaseja


Kutoka kulia kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi, kiungo wa Coastal Union, Uhuru Suleiman ma mwigizaji Elizabeth Michael 'Lulu'


Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Ally Mayay kulia akiwa na Kaburu
POSTED BY:Emanueli O. Ndanshau


0 comments:

Post a Comment