Katika kujifunza kwa vitendo
somo la uhusiano wa kijamii wanafunzi
wa darasa la Tarangire katika
chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha
wamefanya mkutano ulioonyesha mahusiano
kati ya kampuni na jamii.
Mmoja wa wanafunzi wa
darasa hilo Bi.Mgreth Chigogwe alisema
lengo la mkutano huo ni kuongeza uzoefu kwa wanafunzi waliosoma somo hilo ili
kupata uelewa mpana katika taaluma hiyo ili watakapofuzu waweze kufanya kazi
kwa ufanisi .
Hata hivyo mmoja wa
wakufunzi katika chuo hicho Bi.Prisca Mnzava
amesema kuwa kufanya mazoezi kwa vitendo
ni moja ya njia ya kumjenga
mwanafunzi katika msingi imara pindi wawapo chuoni.
Naye Bw.Elifuraha
Samboto ambaye pia ni Mkufunzi alitoa
wito kwa wanafunzi wanaosoma somo hilo waendelee kutia mkazo katika
mazoezi ya vitendo kwani ni njia ya
mafanikio katika tasnia ya habari.
FUATILIA PICHA:
Mwanafunzi Mtaita Elieth aliyesimama kwenye nafasi ya Afisa mahusianoo wa kampuni akitoa maelezo mbalimbali kuhusu bidhaa inayozalishwa na kampuni yao waliyoitambulisha kwa jina la TARANGIRE. |
Mwanafunzi Gervas Danieli aliyesimama kwenye nafasi ya Mkurugenzi wa kampuni akitoa maelezo mbalimbali kuhusu bi kampuni yake waliyoitambulisha kwa jina la TARANGIRE. |
Baadhi ya wanafunzi mbalimbali wakiwa ni waandishi wa habari walioalikwa siku hiyo. |
Baadhi ya wanafunzi mbalimbali wakiwa ni waandishi wa habari walioalikwa siku hiyo. |
Mwanafunzi Frida Aizack aliyesimama kwenye nafasi ya Afisa Uzalishaji wa kampuni akitoa maelezo mbalimbali kuhusu wingi wa bidhaa inayozalishwa na kampuni ya TARANGIRE. |
Mwanafunzi Sinyatti Simon aliyesimama kwenye nafasi ya Mkemia mkuu wa kampuni ya Tarangire akielezea aina ya madawa wanayotumia kutengenezea sabuni |
0 comments:
Post a Comment