Home
Business
Internet
Market
Stock
Downloads
Dvd
Games
Software
Office
Parent Category
Child Category 1
Sub Child Category 1
Sub Child Category 2
Sub Child Category 3
Child Category 2
Child Category 3
Child Category 4
Featured
Health
Childcare
Doctors
Uncategorized
Wednesday, April 30, 2014
Ukawa kuunguruma leo Zanzibar
1:58 AM
No comments
Dar es Salaam.
Hatimaye mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata baraka za polisi.
Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Aprili 19, mwaka huu lakini ukazuiwa na polisi kwa maelezo kuwa intelijensia yao ilionyesha kuwa kungekuwa na tishio la maisha ya watu. Hivyo walishauriwa wapange tarehe nyingine baada ya Sikukuu ya Pasaka.
Hata Aprili 23 ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwa mkutano huo, ilikataliwa na polisi kwa madai kwamba askari na maofisa wa jeshi hilo walikuwa Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yaliyofanyika Aprili 26, mwaka huu.
Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina amethibitisha kuruhusiwa kwa mkutano huo na kuwataka wananchi watakaohudhuria kuwa watulivu kabla na baada ya mkutano.
“Tumewaruhusu kufanya mkutano huo lakini maandamano hayataruhusiwa kufanyika,” alisema Mhina.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema mkutano huo utakaoanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, utahudhuriwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Freeman Mbowe na Dk Willibrod Slaa wa Chadema, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Dk Emmanuel Makaidi wa NLD.
Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wawakilishi 10 kutoka kundi la 201 na wanachama mbalimbali kutoka umoja huo.
“Tunakwenda kuwaelimisha wananchi nini maana ya Katiba, jinsi ya kulinda maoni yao waliyoyatoa yasichakachuliwe na kuwaeleza kwa nini tuliamua kutoka bungeni,” alisema Mtatiro na kuongeza:
“Kesho (leo) tunafanya mkutano Unguja na keshokutwa (kesho) Pemba na tutatoa ratiba ya mikutano mbalimbali itakayofanyika Tanzania Bara kwa makundi tofauti.” Aprili 16 mwaka huu, Ukawa wakiongozwa na Profesa Lipumba walisusia Bunge la Katiba na kutoka nje kwa madai ya kutokuridhishwa na mienendo ya mjadala ya Bunge hilo.
Baada ya kutoka bungeni, walitangaza kufanya mikutano nchi nzima wakianzi
a Zanzibar.
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Newer Post
Older Post
Home
0 comments:
Post a Comment
Social Profiles
Popular
Tags
Blog Archives
UJASIRIAMALI NI MKOMBOZI WA MAISHA..ARUSHA
Mkurugenzi wa mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha bwana Joseph Mayagila Akifungua semina ya ujasiriamali iliyo...
Liberia kupatiwa dawa ya majaribio ya Ebola
Liberia imetangaza kuwa hivi karibuni itapokea dozi za dawa za majaribio ya kutibu ugonjwa wa Ebola kutoka Marekani, ambazo itazitumia kw...
CLUB YA WAANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA WATEMBELEA VITUO VINNE VYA REDIO!!
Picha na Habari by:Emanueli onesmo ndanshau Wanachama wa Club ya Waandishi wa Habari na utangazaji (AJTC) katika Chuo cha Uandishi wa...
WANAHABARI WATAKIWA KUWAFICHUA WANAOUZA DAMU MAHOSPITALINI!!
Mtaalamu kutoka tume ya uchangiaji damu salama Nchini Bw.George Chambo akitoa utambulisho mfupi wa msafara aliofuatana nao. Kat...
KWELI SHETANI AKIZEEKA ANAKUWA MALAIKA
ROONEY APEWA UNAHODHA WA ENGLAND. habari na YASINTA PETER Nahodha mpya wa England Wayne Rooney. Kocha mkuu wa ti...
(no title)
wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari arusha wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya shoo ya pamoja katika maafali ya chuo katik...
MTOTO WA MAREHEMU TYSON "SONIA" ATOA WOSIA MZITO KUHUSU KIFO CHA BABA YAKE, SIKILIZA SAUTI YAKE HAPA
Juzi simanzi ma majonzi vilitawala katika viwanja vya Leaders Club wakati mamia ya watu walipokuwa wakiaga mwili wa muongozaji ...
(no title)
Waraka wa Katiba wa CCM hadharani Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.PICHA|MAKTABA NA SIA MINJA CHANZO MWA...
WAJASIRIAMALI WADOGO KATIKA SOKO LA KWA MROMBO WAMELALAMIKIA UONGOZI WA SOKO HILO KUTOKANA MFUMUKO WA BEI.
(Kutoka kushoto ni mjariliamali MAMA ABDULY ak...
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA MWAKA LA WAKAGUZI WA HESABU ZA NDANI JIJINI ARUSHA LEO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Kongamano la mwaka l...
Powered by
Blogger
.
About Me
Unknown
View my complete profile
Blog Archive
▼
2014
(183)
►
October
(2)
►
September
(17)
►
August
(22)
►
July
(9)
►
June
(19)
▼
April
(11)
AJALI YA BASI LA SUMRY YAUA 22 WAKIWEMO POLISI WAN...
Ukawa kuunguruma leo Zanzibar
Sudan Kusini kujadiliwa hatima yao kujiunga na EAC...
MELI YENYE ABIRIA 460 IMEZAMA KOREA KUSINI
KUHUSU BOMU LA ARUSHA POLISI WATANGAZA BINGO KWA A...
PAMOJA NA MAFURIKO YALIYOPO JIJINI DARESALAAM WATU...
TIZAMA HAPA Yaliyojiri katika Bunge la Katiba
PITIA HAPA KUJUA HATUA ZA MWISHO ZA MZEE GURUMO KA...
MZEE WA MIAKA 60 AUWAA KINYAMA KWA TUHUMA ZA USHIR...
HABARI ZA SHINYANGA: Wimbi la Mauaji ya Vikongwe S...
HABARI ZA IRINGA: WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KWA...
►
March
(31)
►
February
(67)
►
January
(5)
►
2013
(28)
►
December
(5)
►
November
(16)
►
October
(7)
Labels
BURUDANI
habari
habari ya kimataifa
habari ya kitaifa
HABARI ZA BIASHARA
HABARI ZA BUNGE
habari za kimataifa
i
KIJAMII
kitaifa
MICHEZO
Urembo ( fashion).
Blog Archive
▼
2014
(183)
►
October
(2)
►
September
(17)
►
August
(22)
►
July
(9)
►
June
(19)
▼
April
(11)
AJALI YA BASI LA SUMRY YAUA 22 WAKIWEMO POLISI WAN...
Ukawa kuunguruma leo Zanzibar
Sudan Kusini kujadiliwa hatima yao kujiunga na EAC...
MELI YENYE ABIRIA 460 IMEZAMA KOREA KUSINI
KUHUSU BOMU LA ARUSHA POLISI WATANGAZA BINGO KWA A...
PAMOJA NA MAFURIKO YALIYOPO JIJINI DARESALAAM WATU...
TIZAMA HAPA Yaliyojiri katika Bunge la Katiba
PITIA HAPA KUJUA HATUA ZA MWISHO ZA MZEE GURUMO KA...
MZEE WA MIAKA 60 AUWAA KINYAMA KWA TUHUMA ZA USHIR...
HABARI ZA SHINYANGA: Wimbi la Mauaji ya Vikongwe S...
HABARI ZA IRINGA: WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KWA...
►
March
(31)
►
February
(67)
►
January
(5)
►
2013
(28)
►
December
(5)
►
November
(16)
►
October
(7)
Recent Posts
Unordered List
Download
0 comments:
Post a Comment