NICE MEDIA WORKS

KWA WAIMBAJI WA INJILI

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, April 30, 2014

Ukawa kuunguruma leo Zanzibar

 

Wednesday, April 16, 2014

KUHUSU BOMU LA ARUSHA POLISI WATANGAZA BINGO KWA ATAKAYEFANIKISHA KUKAMATWA KWA WALIPUAJI NIGHT PARK


Jeshi la Polisi nchini limetangaza zawadi ya Sh. milioni 10 kwa atakayewezesha kukamatwa kwa  watu waliotumia mabomu kulipua  baa ya Night Park mwishoni mwa wiki iliyopita. Katika mlipuko huo, watu 17 wameripotiwa kujeruhiwa kati ya hao, waliobaki wodini kuendelea na matibabu ni nane baada ya wengine kuruhusiwa.Wanaondelea na matibabu ni  Evance Maleko, Evarist Richard, Petro James, Christian Zakaria, Pius Shayo, Antelus Ishengoma, Sudi Ramadhani na Mariam Hansi aliyeko hospitali ya Selian.Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Isaya Mngulu, alisema uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo umebaini kuwa bomu lililolipuliwa Aprili 13, mwaka huu, saa 1:30 asubuhi kwenye baa hiyo, ni la kutengenezwa kienyeji.Mngulu alisema wataalamu wa mabomu waligundua bomu lingine lililokuwa kwenye mkoba ulioegeshwa kwenye kiti katika baa ya Washington,  pembeni mwa baa hiyo. “Bomu hili tumeligundua baada ya tukio hili kutokea na saa sita usiku tukaligundua, lakini halijalipuka na tunalo kwa ajili ya kuchunguza tujue limetengenezwa kwa kutumia vifaa gani,” alisema.Alisema hata  bomu hilo ni la kutengenezwa kienyeji, jambo lililowafanya waelewe hata hilo lililolipuka ni la kienyeji.Mngulu alisema kutokana na kukithiri kwa matukio hayo nchini kwa sasa, ni vema wananchi na hasa wale ambao wapo maeneo ya mkusanyiko, wakachukua tahadhari za uhakika, kwani siyo vema kumwamini hata rafiki yako.“Ni vizuri ukajiridhisha alichobeba rafiki yako kwenye mkoba na ukitilia wasiwasi bora utoe taarifa polisi na siyo kukaa kimya hadi madhara yakatokea,” alisema.Alitoa rai kwa wamiliki wa kumbi za starehe, makanisani, misikitini na maeneo ya mikusanyiko kujitahidi kuweka kifaa cha CCTV ili kuwezesha kubaini wahalifu pale uuhalifu unapotokea.Alisema hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kwa kuwa wana kifaa cha CCTV kilichofungwa Night Park, wana hakika muhusika atapatikana. Alisema matukio ya milipuko ni mengi kutokea nchini kwa sasa na yanatokea maeneo mbalimbali na siyo Arusha peke yake, isipokuwa wote wanaokamatwa na milipuko hiyo kama Dar es Salaam na Tanga ni vijana wadogo ambao hawajawahi hata kupita jeshini.Kuhusu Sikukuu za Pasaka, alisema kila mkoa umepewa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi kutumia mbinu zao zote na vifaa walivyonavyo kama farasi na mbwa ili kulinda usalama wa ibada za sikukuu hizo.

Tuesday, April 15, 2014

PITIA HAPA KUJUA HATUA ZA MWISHO ZA MZEE GURUMO KABLA YA MAUTI KUMFIKA


http://gopaidweekly.com/?ref=80557

Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi nchini, Muhidini Maalim Gurumo aliyefahamika pia kama kamanda na mashabiki wa muziki wa dansi, aliyeaga dunia Jumapili iliyopita katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar, alikutana na mateso ya kwa saa 72 za mwisho wake baada ya kulazwa akiwa taabani kwa siku tatu.

Mtoto wa marehemu anayejulikana kwa jina la Abdalah aliliambia Uwazi kuwa siku mauti yalipomfika baba yake katika wodi namba sita Jengo la Mwaisela, alimtembelea na kumkuta akiwa katika hali nzuri na alipopewa chakula alikula, akashiba lakini cha ajabu alisema hatakula tena.
Kijana huyo alisema muda mfupi baadaye, hali ya baba yake ilibadilika, akaanza kupumua kwa shida ndipo alipozidiwa na baadaye kukata roho.

Mzee Gurumo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa mapafu kwa muda mrefu na aliwahi kulazwa katika hospitali hiyo ya Muhimbili.
Baadhi ya watu waliomtembelea mzee Gurumo kwa nyakati tofauti akiwa hospitalini hapo ni pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alimuombea afya njema na akaruhusiwa kurudi nyumbani.


Kifo chake kimeacha simanzi si tu kwa familia yake, bali kwa wadau wa muziki wa dansi kwani alikuwa mwalimu na kiongozi wa wanamuziki wengi ambao sasa wanatamba.
Baada ya kustaafu muziki, Mzee aliwahi kupewa zawadi ya gari na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ aina ya ToyotaFuncargo. Akizungumzia msiba huo, Kiongozi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki alisema wamempoteza mwalimu wa muziki asiyekuwa na choyo ya kuelimisha.


“Ni kama tumepoteza tochi tukiwa kwenye msitu mnene usiku wa manane,” alisema.

Naye msemaji wa Bendi ya Mlimani Park Ochestra (Sikinde Ngoma ya Ukae), Jimmy Chika alipozungumza na Uwazi alisema mzee Gurumo aliwahi kuja kuwatembelea na kuimba mwezi mmoja uliopita katika Ukumbi wa DDC, Kariakoo jijini Dar.

“Alikuja kama mara tatu hivi ukumbini, naona alikuwa kama anatuaga kwa sababu alikuwa mwanzilishi wa bendi na mbunifu wa mtindo wa Sikinde, aliubuni Septemba, 1978,” alisema Chika.Mzee Kassim Mapili, mwanamuziki wa mkongwe, kwa upande wake alisema kifo cha Gurumo ni pengo kubwa ambalo haliwezi kuzibika na akafafanua kuwa ni mtu ambaye hakuwa mbinafsi.

Baadhi ya wanamuziki ambao amefanya nao kazi kwa karibu ambao sasa watakuwa wanamlilia mwalimu wao ni pamoja na Hassan Rehani Bitchuka, Said Mabela, Roman Mng’ande ‘Romario’ na wengine wengi. Gurumo pia ameacha simanzi katika miji mbalimbali nchini kwa kuwa amewahi kutembelea kimuziki na alifanikiwa kujizolea mashabiki lukuki.

Hadi Uwazi linakwenda mitamboni msiba ulikuwa nyumbani kwake Mabibo, Dar huku taratibu za mazishi zikifanyika. Ameacha mjane na watotowanne. 

MZEE WA MIAKA 60 AUWAA KINYAMA KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA HUKO MAKETE!!!!! Daktari Luvanda kutoka hospitali ya wilaya ya Makete akionesha majeraha ya kichwa cha mwili wa marehemu yanayohisiwa kupelekea kifo chake. Mwili wa marehemu baada ya kuondolewa eneo la tukio. Polisi kutoka kituo cha Tandala na Makete wilayani wakichukua taarifa za mauaji hayo kwenye shamba ulipokutwa mwili wa marehemu. Askari akizungumza na wananchi waliofika eneo la tukio na kuwaonya kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi pamoja na kushirikiana na jeshi hilo kuwapata watuhumiwa wa mauaji hayo. Mkazi wa kijiji cha Masisiwe kata ya Ukwama Wilayani Makete Mkoani Njombe amefariki Dunia baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mguuni na mtu/watu wasiojulikana mwishoni mwa wiki iliyopita Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya, Mrakibu mwandamizi wa Polisi ambaye pia ni afisa upelelezi Wilaya ya Makete Bw.Gozbert Komba amesema walipokea taarifa ya mauaji hayo kutoka kwa uongozi wa kijiji hicho na kumtaja marehemu kuwa ni Masori Sanga(60) mkazi wa kijiji cha Masisiwe Kata ya Ukwama Wilayani Makete Bw. Komba amesema kuwa marehemu huyo aliuawa usiku wa kuamikia Ijumaa wiki iliyopita na watu wasiojulikana kwa imani za kishirikina kwa kuwa marehemu alikuwa mzee na pia kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda wa tukio hilo waliohojiwa na polisi Pia amesema mpaka sasa Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kwa ajili ya kuhakikisha wahusika wote wa tukio hilo wanakamatwa kwani kitendo walichokifanya ni cha kinyama na baada ya tukio hilo muuaji/wauaji hao walitokomea kusiko julikana Bw.Komba amekemea vikali suala la wananchi kujichukulia sheria mkononi wilayani hapo na kuwaomba wananchi wasiwe na tabia hizo za kuwaua wazee kwa imani za kishirikina na kuwataka watii sheria bila shuruti ili kuishi kwa Amani katika wilaya yao na nchini kwa ujumla Mwili wa marehemu ulikutwa kwenye shamba la mahindi ukiwa na majeraha sehemu za kichwani na mguuni ambayo yanadhaniwa kusababisha kifo chake, baada ya watu kupita eneo hilo na kuukuta mwili huo katika kipindi cha hivi karibuni wilayani Makete kumekuwa na matukio ya mauaji kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo wivu wa kimapenzi na imani za kishirikina jambo linalotia doa wilaya hiyo kutokana na ongezeko la watu kuchukua sheria mikononi kwa kuwaua watuhumiwa wa matukio mbalimbali











Friday, April 4, 2014

HABARI ZA SHINYANGA: Wimbi la Mauaji ya Vikongwe Shinyanga lapungua!