Tuesday, October 29, 2013

CAPITAL ONE CUP: ARSENAL NJE, CHELSEA, MAN UNITED ZIPO ROBO FAINALI!


 ROBO FAINALI KUFANYIKA JUMATANO USIKU!!
CHELSEA imeitwanga Arsenal waliokuwa kwao Emirates Bao 2-0 na kutinga Robo Fainali yaCAPITAL_ONE_CUP-BESTCAPITAL ONE CUP pamoja na Manchester United ambao waliwatandika Norwich City Bao 4-0 Uwanjani Old Trafford.
Timu nyingine ambazo zimetinga Robo Fainali baada ya kushinda ni West Ham na Licester City.
Mechi kato ya Birmingham na Stoke City ilikuwa Sare ya Bao 3-3 katika Dakika 90 na ikaingia kwenye Dakika 30 za Nyongeza na Matokeo kuwa 4-4 lakini Stoke City wamesonga kwa Penati 4-2.


RAUNDI YA 4
MATOKEO:
Jumanne Oktoba 29
Arsenal 0 Chelsea 2
Birmingham 3 Stoke 3 [Dakika 30 za Nyongeza Bao 4-4, Penati Stoke yashinda 4-2]
Burnley 0 West Ham 2
Leicester 4 Fulham 3
Man Utd 4 Norwich 0

ARSENAL 0 CHELSEA 2
Arsenal wakiwa kwao Emirates wamepigwa Bao 2-0 na Chelsea na kutupwa nje ya Capital One Cup.
Bao za Chelsea zilifungwa na Azpilicueta katika Dakika ya 25 na Juan Mata kwenye Dakika ya 66.
VIKOSI:
Arsenal: Fabianski; Jenkinson, Vermaelen, Koscielny, Monreal; Ramsey, Wilshere, Rosicky, Cazorla, Ryo; Bendtner
Akiba: Viviano, Sagna, Hayden, Yennaris, Ozil, Giroud, Park.
Chelsea: Schwarzer; Azpilicueta, Cahill, David Luiz, Bertrand; Essien , Mikel; De Bruyne, Mata, Willian; Eto’o
Akiba: Blackman, Ivanovic, Kalas, Ramires, Hazard, Torres, Ba.
Refa: Phil Dowd.
MAN UNITED 4 NORWICH CITY 0
Bao za Javier Hernandez ‘Chicharito’, Bao mbili, moja likiwa la Penati baada ya Januzal kuchezewa rafu, Phil Jones na Fabio, zimewapa Man United ushindi wa Bao 4-0 walipoichapa Norwich City Uwanjani Old Trafford.
Ushindi huu umeipeleka Man United Robo Fainali ya Capital One Cup.
VIKOSI:
Manchester United: Lindegaard; Rafael, Ferdinand, Vidic, Buttner, Zaha, Cleverley, Jones, Young, Januzaj, Hernandez.
Akiba: Amos, Anderson, Rooney, Giggs, Smalling, Fabio and Valencia.
Norwich: Bunn; Whittaker, R. Bennett, Bassong, Garrido; Snodgrass, Fer, Johnson, Redmond; Hoolahan; Elmander
CAPITAL ONE CUP
RAUNDI YA 4
RATIBA
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku]
Jumatano Oktoba 30
Newcastle v Man City
Tottenham v Hull   
Jumatano Novemba 6
Sunderland v Southampton

DONDOO MUHIMU:
-KLABU 92 za BPL [Klabu 20] na Ligi za Madaraja Matatu ya chini [Championship, Ligi 1 na 2, Jumla Klabu 24 kila Ligi] hushiriki Raundi 7 za Mashindano.
-NUSU FAINALI huchezwa kwa Mtindo wa Mtoano wa Nyumbani na Ugenini.
-KLABU ZA BPL HUANZA kushiriki Raundi ya Pili lakini zile ambazo zinacheza Mashindano ya UEFA ya CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI huanza kucheza Raundi ya Tatu.
-FAINALI ITACHEZWA TAREHE 2 MACHI 2014 Uwanja wa Wembley na Bingwa hushiriki UEFA EUROPA LIGI Msimu unaofuata.
-MFUMO:
Raundi ya 1: Wiki ya kuanzia Agosti 5
Raundi ya 2: Wiki ya kuanzia Agosti 26
Raundi ya 3: Wiki ya kuanzia Septemba 23
Raundi ya 4: Wiki ya kuanzia Oktoba 28
Raundi ya 5: Wiki ya kuanzia Desemba 16
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: Wiki ya kuanzia Januari 6
Nusu Fainali-Marudiano: Wiki ya kuanzia Januari 20
Fainali: Jumapili 2 Machi 2014
@Soka in Bongo.
POSTED BY:Emanuel Onesmo Ndanshau

0 comments:

Post a Comment