NICE MEDIA WORKS

KWA WAIMBAJI WA INJILI

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, September 10, 2014

ARUSHA;WANAFUNZI WAISHIO HOSTELI AJTC WATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA....

 Aliyeva shati jeupe ni Waziri Emmanuel Ndenshau kiongozi wa hosteli za Loliondo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha akihojiwa na mwandishi wa blog hii Gift Adison.picha na TEODORA MASSAWE.


Baadhi ya wanafunzi wa hosteli wakiwa katika eneo la kantini..picha na TEODORA MASSAWE.



Baadhi ya wanafunzi wa hosteli wakiwa wanajisomea katika eneo la hosteli..picha na TEODORA MASSAWE.


Habari na GIFT ADISON,
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha wanaoishi hosteli za loliondo wameomba uongozi wa hosteli hiyo kuwapatia vifaa vya kufanya usafi kwa wakati ili kuweka mazingira safi.

Wakizungumza na waandishi wa habari mapema leo wamesema kuwa wamekuwa wakicheleweshewa vifaa vya kufanya usafi kitendo kinachowapelekea mazigira ya hosteli hiyo kotoridhisha.

Mmoja kati ya wanafunzi hao aliyejitambulisha ZIARA NYATU amesema kuwa maisha ya hosteli ni mazuri endapo mazingira yatakuwa safi ili kuwaepusha na magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu
   ``Maisha ya hositeli yananisaidia kuwa huru kitaaluma kwani nakuwa na muda  mwingi wa kubadilishana  mawazo na wezangu na kufanya mazoezi ya vitendo katika kituo cheti cha redio hapa chuoni ``Alisema nyatu.
                   
 Pia ameeleza changamoto wanazokabiliana nazo  kuwa ushirikiano hafifu kwa wanafunzi wengine kawa kutoshiriki katika ufanyaji usafi, tabia ya wizi, uhaba wa maji safi ya kunywa, na pia kuwapelekea baadhi ya wanafunzi kuzidi kuhama kutoka katika hosteli

``wanafunzi wengi wanatoka sehemu mbalimbali kila mtu akiwa na tabia yake hivyo inachukua mda kumbadilisha mtu kuendana na mazingira Fulani ambayo hajayazoea kama vile kufannya usafi wa jumla, na kuchoma taka pale zinapoonekana kujaa`` alisema nyatu 
  
Kwa upande wa kiongozi wa hosteli ya loliondo bwana Emmanuel Ndanshau amesema kuwa amekuwa akifanya vikao  chumba hadi chumba ili kuweza kuwashauri na kuwaonya pale wanapokwenda kinyume sheria na utaratibu wa hosteli

Bwana Ndanshau ameeleza matatizo anayokumbana nayo katika mazingira hayo ni gari la taka kuchelewa kufika kwa wakati pamoja na uhaba wa maji safi ya kunywa ingawa maji yanayopatikana ni ya kisima kwani sio bora kwa afya zao




  

ARUSHA;WANAFUNZI AJTC KUANZA MITIHANI SEPTEMBA 15 HADI 19 MWAKA HUU


Mwanafunzi Eveline Molel[Kulia], akifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa blog hii Evelyine Bakari[kushoto]katika moja ya darasa ndani ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.picha na YASINTA PETER.


Mwanafunzi Yusuph Mbata Akijisomea Kujiandaa na Mtihani,picha na YASINTA PETER

Habari na EVELYINE BAKARI                                                               
Wanafunzi wa darasa la Ruaha katika chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Arusha wanatarajia kufanya mitihani  ya kumaliza muhula wa kwanza kuanzia tarehe 15 mpaka tarehe 19 mwezi wa tisa mwaka huu.

Wakizungumza  na AJtc  mapema jana wanafunzi hao wamesema kuwa wamejiandaa vizuri na mitihani na wanatarajia kufaulu vizuri katika masomo yote, akizungumzia suala hilo mwanafunzi wa darasa hilo Evelyn Mollel alikuwa na haya ya kusema,

‘’Nimejiandaa vizuri na mtihani ambao tutaanza tarehe 15 mpaka tarehe 19 na ninatazamia kufaulu vizuri katika masomo yote na nina hakika  na wanafunzi wenzangu wamefanya hivyo.

Kuhusu suala la mtaala mpya wanafunzi hao wamesema ,mtaala huo ni mzuri kwa kuwa unawawezesha kujua na kupata muongozo wakati wanasoma pindi wanapokaribia kufanya mitihani kwa kuwa wanasoma mitihani waliyopewa madarasa mengine hivyo hawapati shida kufikiria wapi pa kusoma.

 Wakielezea changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni pamoja na ukosefu wa ushirikiano kati ya wanafunzi wa darasa hilo na wengi wao kutoroka darasani kabla ya muda wa kuondoka pamoja na kubadilishiwa tarehe ya kufanya mtihani.

Pia wanafunzi hao wamemalizia kwa kuwaasa wanafunzi wenzao wa madarasa mengine  kusoma kwa bidii na waache mambo mengine na kuzingatia masomo.




WAJASIRIAMALI WADOGO KATIKA SOKO LA KWA MROMBO WAMELALAMIKIA UONGOZI WA SOKO HILO KUTOKANA MFUMUKO WA BEI.









(Kutoka kushoto ni mjariliamali MAMA ABDULY akizungumza na na mwaandishi wa habari mapema jana)

Mmoja wa wa mfanya biashara katika soko hilo aliyejulikana kama ,MAMA ABDULY akizungumza na waandishi wa habari hapo jana  katika sokoni hapo nakusema kupanda kwa bei za nyanya pamoja na mboga ni changamoto kwao kwani wanashindwa kukidhi mahitaji yao pamoja na familia zao

Alisema kuwa wamekuwa wakinunua sanduku (tenga) moja kwa bei ya shilingi eilfu tisa(9000) mpaka eilfu ishirini na mbili(22000) lakini kwa sasa wananunua kwa shilingi (25000) mpaka sh.30000 kwa bei ambayo inaleta changamoto wakati wakuwauzia wateja wao kwani wanashindwa kuelewana.

"Mteja aliyezoea kununua nyanya kwa bei nafuu alafu anakuta bei imepanda  mpaka kumuelewesha inachukua mda kwa sababu anakuta nyanya za mia tano ni nne(4) na amezoea kwa kukuta ni nyanya sita au saba anashindwa kuelewa" alisema mama abduly.

Aidha mjasiriamali huyo aliweza kuzungumzia biashara nyingine ya mboga  kwani wakulima walikuwa wanawauzia mboga fungu moja sh.100 lakin sasa wanawauzia fungu 3 kwa shilingi mia tano.(500) bei ambayo ni kikwazo kwao.

"kama unavyoona sijasoma sana na nimeamua kujishughulisha na biashara hii ya uuzaji wa nyanya na mbogamboga kwa kukidhi mahitaji yangu       pamoja na familia yangu pia nasomesha watoto kupitia biashara hii,nimenunua kiwanja kupitia biashara hii ambapo ni faida nayoipata lakini sasa nashindwa  kupta faida kutokana na bei hizikabisa",alisema

Pamoja na hayo wafanya biashara hao wameendelea kusema kuwa 
changamoto hizo zinaambatana nakutokuwepo kwa choo,maji kwani ni huduma muhimi sanak wa jamii pamoja na sehemu maalum ya kufanyia biashara hizo kwani eneo hilo ambalo ni wanalitumia kwa sasa limekuwa dogo kutokana kuwa na wafanya biasharakatika eneo hilo.

Pia wafanya biashara hao walimazia kwa kusema wanauomba uongozi wa soko hilo kuwatengea eneo maalum kwa ajili ya biashara hiyo kwani eneo hilo wnaolifanyia biashara ni changamoto kwao na dogo sana kwani eneo hilo liko kandokandona barabara ikiwa nia hatari kwa maisha yao..HABARI NA ELIZABETH NJAU,PICHA NA GEORGE HILONGA



Tuesday, September 9, 2014

WANAFUZI WA AJTC WAASWA KUWA NA MWITIKIO KWENYE MASHINDANO YA UTANGZAJI

Mkuu wa idara ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaziji arusha bwana Onesmo Elia Mbise akifanya  maojiano na mwanishi wetu (picha na mwanaidi omary)


Mkuu wa idara ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaziji arusha bwana Onesmo Elia Mbise amewaasa wanafunzi wa chuo hicho kuwa na mwitukio pindi yanapotokea katika mashindano ya utangazaji
Amesema dhumuni la mashindano hayo ni kuinua vipaji vya utangazaji  na kuimarisha wanafunzi katika uandaji wa vipindi wa radio na Tv

Monday, September 1, 2014

ujerumani kuwapatia sila wakurd


Ujerumani inatarajia kulitumia jeshi la Wakurd wa Iraq silaha ikiwemo bunduki na silaha zile zenye mfumo unaoweza kukabiliana na mashambulizi ya vifaru vya kivita.
Jeshi hilo limekuwa likipambana na wapiganaji wa kiislamu kaskazini mwa Iraq.

Amesema uamuzi huo ni kutokana na maslahi ya nchi yake.Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula Von der Leyen amesema silaha hizo zotaweza kuwatosheleza wanajeshi elfu nne ifikapo mwishoni mwa Septemba.
Hatua hiyo iliyochukuliwa na Ujerumani imeelezwa kuwa ni ya nadra sana kwa nchi hiyo, kupeleka silaha kwenye eneo lenye mapigano.
Hata hivyo uamuzi huo umekosolewa na baadhi ya watu ambao wana wasiwasi zitakapoishia silaha hizo.                                                                                                 na mwandishi wako kennedy rutta

TULIPOFIKIA TUSIRUHUSU TENA SIASA IENDESHE UCHUMI =



 Katika utawala wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa na uchumi huria, kuendeleza mfumo uleule wa kizamani katika medani ya siasa, mathalan, dhana ya “chama tawala”; “chama kushika hatamu za uongozi”; “chama kimoja”; “zidumu fikra za mwenyekiti”, kwa moyo wa dhati kabisa, lazima niseme kwamba, kwa mtindo huo, Watanzania tutajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe.


Mabadiliko au mageuzi ya kiuchumi tuliyoyatarajia hayatakuwepo asilani . Nchi za wenzetu duniani, na hata za majirani zetu, zitasonga mbele kiuchumi, tena kwa kasi, lakini sisi tutabakia hapa tulipo, na pengine tukarudi nyuma zaidi kimaendeleo.

Kwa sababu, sisi tutakaposinzia, tutawapa mwanya wenzetu wa nje waje zaidi kuwekeza nchini. Wachote zaidi kilichopatikana, na kukipeleka kwao, wakituacha na umaskini wetu.

Tumekiona hicho kikifanyika katika sekta ya madini na rasilimali nyingine za nchi, ambazo Watanzania wenyewe hawakuwa na ubavu wa kuwekeza vilivyo.
Ukweli ni kwamba Watanzania tutaendelea kujikongoja kwa mwendo wa Konokono, tukiomba Mungu tusipishane na gari yanayoendeshwa na wawekezaji kutoka nje wenye mitaji mikubwa’.

Watanzania tutabakia tumenasa, na hata ikibidi kuzama zaidi katika lindi la ufukara na umaskini .

Watu hawatakuwa na uwezo wa kuwekeza na kuendesha miradi mikubwa ya kiuchumi yenye uwezo wa kuleta mabadiliko makubwa haraka (BRN), kama wengi walivyotarajia

Kwa nini ? Kwa sababu tutakuwa tumekubali kuruhusu ushindani katika uchumi, yaani nguvu za soko na sekta binafsi ziongoze uchumi na biashara.
Lakini, bado tutakuwa wagumu au tumeshikwa na kigugumizi katika kuruhusu ushindani wa kweli katika medani ya siasa kwa kuruhusu au kukubali kuwa na Katiba mpya itakayoruhusu na kufungua milango ya ushindani wa kisiasa, na Katiba hiyo mpya kuwa mhimili wa kweli wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, kwa kutengeneza uwanja ulio sawa wa ushindani wa kisiasa, miongoni mwa vyama vya siasa nchini, bila kuruhusu ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Wenzetu wamepiga hatua kubwa kiuchumi kwa sababu ya ubora na umakini wa katiba zao. Katiba zao zimejenga ushindani wa kisiasa uliokidhi mahitaji ya ushindani wa kiuchumi .

Kwa kuwa tumekubali ushindani wa kiuchumi, hatuna budi kukubali ushindani wa kweli na wa haki kisiasa. Vitu hivyo viwili daima huenda pamoja, vikiachana lazima patatokea mtafaruku kimaendeleo.

Ziko wapi tena nguvu za umma katika vyama vya siasa, wakati mashirika yao ya umma yaliuawa na wajanja wachache na wao wakaachwa yatima ?
Ziko wapi tena zama za nguvu ya umma, kwa kutoa ahadi za nafasi nyingi zaidi za ajira, na hali bora zaidi ya maisha, wakati viwanda vyao vilipukutika na kubakia maghofu na nchi kugeuzwa dampo la bidhaa duni kutoka nje?
Wakati migodi yote muhimu ikimilikishwa kwa wageni (kampuni za kimataifa), na wao wakibakia na vumbi lisilo na utajiri wa uhakika?
Katika mazingira kama hayo ya uchumi shindani, bila ya kuruhusu siasa shindani itakayoongoza na kulindwa na Katiba mpya na bora, iliyobeba maudhui hayo ya mageuzi ya kiuchumi, basi tujue kwa hakika kwamba Watanzania tutajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe.

Hakuna cha maana kitakachofanyika kiuchumi katika dunia hii ya utandawazi. Utegemezi wa kiuchumi na kiteknolojia utazidi kuongezeka kwa kukosa ubunifu wa kifikra na mawazo mbadala.

habari  na   winlady   johaness  mbesere

Mlipuko waua a mjini Paris.

na GIFT ADISON

Jengo lililolipuliwa

Mlipuko umeharibu jengo moja la ghorofa 4 kazkazini mashariki mwa Paris na kumuua mvulana mmoja huku watu kadhaa wakiwa hawajulikani walipo.
Watano kati ya wale waliotoweka wanadaiwa kuwa watoto.
Afisa mmoja wa huduma ya zima moto katika mji huo mkuu amesema haijulikani ni nini kilichosababisha mlipuko huo.
Msemaji huyo amesema kuwa maafisa wa matibabu wamepelekwa katika eneo hilo.