NICE MEDIA WORKS

KWA WAIMBAJI WA INJILI

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Friday, August 29, 2014

BAADA YA KUCHEZA MIAKA 17 MFULULIZO HATIMAYE ETO'O ASTAAFU KUCHEZEA TIMU YA TAIFA

ETO'O ASTAAFU KUICHEZEA TIMU YAKE YA TAIFA YA CAMEROON. 

NA MWANAIDI K OMARY


                                            Samuel Eto'o akiwa na jezi ya timu yake ya Taifa.

Mshambuliaji mpya wa Everton raia wa Cameroon Samuel Eto’o ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa tangu aanze kuitumikia nchi yake mwaka  1995 ambapo Cameroon ilifungwa magoli 5 kwa 0 na Costa Rica.
 
Eto’o mwenye umri wa miaka 33 amestaafu akiwa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote kwa timu yake ya taifa baada ya kupachika magoli 56 licha ya kutofunga goli lolote kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
 
Mshambuliaji huyo katika historia yake  amevichezea vilabu mbalimbali barani Ulaya kama Real Madrid,Marlloca, Fc Barcelona,Inter Milan, Anzhi Makhachkala,Chelsea,na sasa  anaichezea Everton akijiunga kwa uhamisho huru nakupewa mkataba wa miaka miwili akitokea Chelsea.
 
Akizungumza uamuzi wake wa kustaafu Eto’o ambaye ni kati ya wachezaji wa kiafrika waliowahi kukumbwa na maswahibu ya kubaguliwa kutokana na rangi yake  barani Ulaya amewashukuru waafrika wote hususani masahabiki wake kwa kuumuunga mkono na kumpenda.
Uamuzi wake ametangaza kupitia matandao wa kijamii wa Instagram.

Michezo ya kimataifa aliyocheza tangu 1997-2014 kwenye timu ya taifa ya Cameroon.

Year
Apps
Goals
1997
3
0
1998
5
0
1999
1
0
2000
9
5
2001
9
2
2002
13
5
2003
7
2
2004
9
4
2005
6
1
2006
5
5
2007
3
1
2008
11
11
2009
8
5
2010
12
8
2011
9
4
2012
2
0
2013
4
2
2014
2
1
Total
117
56

KWELI SHETANI AKIZEEKA ANAKUWA MALAIKA

ROONEY APEWA UNAHODHA WA ENGLAND. 

habari na YASINTA PETER



Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson  amemteua mshabuliaji wa Manchester United Wayne Rooney kuwa nahodha mpya  kuchukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na kiungo wa Liverpool Steven  Gerrard aliyestaafu mwezi uliopita.

Rooney mwenye umri wa miaka 28 ameshafunga magoli 40 kwenye timu ya taifa katika michezo 95 aliyocheza  hadi sasa na ataanza kuvaa kitamba cha unahodha kuanzia kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Uingereza na Norway septemba 3 mwaka huu.

Kocha  Roy Hodgson amesema anaamini Rooney anastahili kuwa nahodha wa Uingereza na kuteuliwa kwake kuwa nahodha wa Manchester United hivi karibuni kulidhihirisha kwamba anafaa kwa nafasi hiyo.

Aidha kocha huyo ametangaza kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki mwezi ujao dhidi ya Norway kabla ya kuikabili Uswis Septemba 8 mwaka huu.



Magoli kipa;Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), na Joe Hart (Manchester City) 

Walinzi ni Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Calum Chambers (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Danny Rose (Tottenham Hotspur),na  John Stones (Everton) 

Viungo ni Jack Colback (Newcastle United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal) Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), na Jack Wilshere (Arsenal) 

Washambuliaji ni  Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), na Danny Welbeck (Manchester United

MANJI ASISITIZA, SIMBA WAMEKURUPUKA KWA OKWI

Na Amalia seraphine

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema Simba wamekurupuka katika suala la Emmanuel Okwi.

Tuesday, July 1, 2014

AJTC WAIBUKA KIDEDEA KWENYE BONANZA LA WAANDISHI WA HABARI MKOANI ARUSHA

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo nchini(Taswa)Juma Pinto(kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa kudumu wa Taswa mkoa wa Arusha,Jamila Omary aka "Dangote" wakati wa Bonanza la vyombo vya lililopigwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mgeni Rasmi katika Bonanza la Vyombo vya Habari mkoani Arusha,Juma Pinto wa pili kushoto,akifatilia michezo iliyokua inaendelea kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wengine kushoto ni Le Mutuz,Mkurugenzi wa Gogobichi Media,Joseph Lyimo na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mega Trade,Goodluck Kway

Washindi wa kukimbiza Kuku  kutoka The Institute of Media and Social Studies(IMS) "wakishow"

Katibu wa Kudumu wa Taswa Arusha,Mussa Juma(shoto) akiwa Le Mutuz baada ya kukagua timu za Arusha One Radio na Arusha Journalism Training College(AJTC)

Mabingwa katika mpira wa miguu na mpira wa Pete(Netball)Chuo cha Arusha Journalism Training College(AJTC)wakishangilia ushindi wao.

Waandishi wa habari za michezo wakifatilia burudani.

WAKUFUNZI wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakifuatilia mwenendo wa Mchezo kati ya Sunrise Redio na  Chuo cha  hicho cha AJTC

 
Baathi ya wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakifuatilia kwa makini Mpambano.


Katibu Msaidizi wa Taswa Arusha na Mtangazaji Mahiri wa vipindi vya Michezo na Burudani,Hamza Kalemera akichapa kazi,kulia ni Mussa Juma

Tuesday, February 25, 2014

YANGA YATENGEWA MILION 100 KUWAUWA WAARABU

NA MARYLINE OLOTU
AL AHLY imepanga kuwasili nchini leo Jumanne tayari kuikabili Yanga Jumamosi hii kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini Mwanaspoti linajua kwamba matajiri wa Jangwani wamepanda mzuka na kuwatengea wachezaji wao Sh100 milioni endapo wakishinda mchezo huo.
Yanga itavaana na mabingwa watetezi hao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kisha timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye huko Cairo, Misri.
Yanga ikiwa na kikosi chake kamili kitakachoongozwa na straika matata, Emmanuel Okwi, iko kambini Bagamoyo, Pwani, ikinoa makali.
Ingawa matajiri hao walidai kwamba ahadi yao ni siri mpaka wikiendi, habari za uhakika kutoka kwenye chanzo cha kuaminika ndani ya benchi la ufundi, zimeeleza kuwa fedha hizo zimeahidiwa ili kuongeza morali na kurahisisha mechi ya marudiano ugenini.
Tayari uongozi umewapa wachezaji hao zawadi ya Sh5 milioni baada ya kuichapa Ruvu Shooting mabao 7-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara hivi karibuni.
Yanga ilipanga kuwapa Al Ahly Uwanja wa Karume kwa ajili ya mazoezi, lakini timu hiyo ikagoma na yenyewe ikaomba viwanja vya Gymkhana na Azam Complex ambako kote wamegonga mwamba hadi walipobahatika kwenye Uwanja wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST).
Mechi ya Dar es Salaam itachezeshwa na Bazezew Belete wa Ethiopia na ya marudiano itachezeshwa na Mohamed Ragab wa Libya ambaye atasaidiwa na Fouad Fathi Farag kutoka Morocco.