Showing posts with label kitaifa. Show all posts
Showing posts with label kitaifa. Show all posts
Friday, August 29, 2014
TANZANIA NA BURUNDI ZAIMARISHA ALAMA ZA MIPAKA YAKE.....
Shughuli ya kuweka alama mpya ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi inaendelea, ambapo nchi hizo mbili jirani zinapima na kuweka mawe ya kimataifa kati ya mipaka.
Hafla rasmi ya zoezi hilo ilizinduliwa jana upande wa Tanzania katika kijiji cha Mugikomelo mpakani mwa nchi hizo mbili na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa nchi mbili. Katika hafla hiyo Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amewashukuru Watanzania wote kwa mchango wao mkubwa katika kueleta amani na utulivu katika nchi yake, akisisitiza kuwa, licha ya nchi mbili hizo kuwa na mpaka lakini Tanzania inaruhusu maelfu ya wakimbizi wa Burundi kuingia nchini kwake bila kufuata taratibu za mipaka na uhamiaji, kwa sababu ya matatizo yanayowakabili Warundi.
Uwekaji mawe kwenye mpaka wa kimataifa kati ya nchi hizo mbili, unafanyika ikiwa ni baada ya kukamilika mchakato mrefu uliohusisha wataalamu wa nchi hizo wa kupima theluthi moja tu ya mpaka huo wa nchi mbili wenye kilometa 451.
Mpaka wa Tanzania na Burundi ni wa tano kwa urefu kati ya nchi 8 jirani na Tanzania, huku Kenya ikiwa na mpaka mrefu zaidi wenye kilometa 769.
CHANZO: BBC
HABARI NA STEVEN MULAKI
Thursday, August 21, 2014
ANGALIA WANAFUNZI WA AJTC WAKIWA KATIKA MAZOEZI YA VITENDO
| Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha AJTC wakisikiliza moja ya presentation zilizokwa zikitolewa na wanafunzi wenzao hii ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo |
| Mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho Bahati Mshana akiwasilisha mada yake mbele ya wanafunzi |
| somo la Public raations likiwa linawasilishwa kwa vitendo na baadhi ya wanafunzi chuoni hapo |
Thursday, July 3, 2014
Kova:wawili wakamata kuhusika na mauaji ya sister
na Alicia sebastian
“Majambazi hao walikamatwa kutokana na operesheni kali inayoendelea jijini hasa baada ya kifo cha sista huyo” Kamanda Kova
na alicia sebastian
KWA UFUPI
- Mmoja alikuwa dereva wa bodaboda iliyokuwa imembeba jambazi aliyetoroka na fuko la fedha na mwingine alikuwa kiongozi wa tukio hilo.
Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata watu wanane na kati ya hao, wawili wakidaiwa kuhusika na mauaji ya Sista wa Kanisa Katoliki, Cresencia Kapuri na wengine, uporaji wa Benki ya Barclays, Tawi la Kinondoni.
Watuhumiwa hao wawili wanadaiwa kuwa, Juni 23, mwaka huu walifanya mauaji ya Sista huyo eneo la Riverside, Ubungo, Dar es Salaam na kupora kiasi cha Sh20 milioni na nyaraka mbalimbali.
Katika tukio jingine la Aprili 15, mwaka huu watuhumiwa wengine wanadaiwa kupora Sh500 milioni za benki ya Barclays.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema majambazi hao walikamatwa kutokana na operesheni kali inayoendelea jijini hasa baada ya kifo cha sista huyo.
Kamanda Kova alisema watuhumiwa waliokamatwa kuhusiana na mauaji ya mtawa huyo wa Kanisa Katoliki, mmoja alikuwa akiendesha bodaboda na alimbeba jambazi mwenzake akiwa na fuko la mamilioni ya fedha na kutoroka nalo wakati mtuhumiwa wa pili aliyekamatwa ambaye ni mfanyabiashara, ndiye aliyekuwa kiongozi katika tukio hilo.na Alicia sebastian
na romana chuwa
IBADA MAALUM: Maaskofu wawataka Ukawa kurejea bungeni
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) ambaye pia ni Askofu wa Jimbo la Iringa, Tarcisius Ngalalekumtwa kwenye Uwanja wa Kichangani Manispaa ya Iringa jana wakati wa jubilei yake ya miaka 25 ya uaskofu. Picha na Hakimu Mwafongo na romana chuwa
KWA UFUPI
- Baraza la Maaskofu limewataka Ukawa kurejea bungeni bila masharti yoyote.
KITAIFA
IBADA MAALUM: Maaskofu wawataka Ukawa kurejea bungeni
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) ambaye pia ni Askofu wa Jimbo la Iringa, Tarcisius Ngalalekumtwa kwenye Uwanja wa Kichangani Manispaa ya Iringa jana wakati wa jubilei yake ya miaka 25 ya uaskofu. na romana chuwa
Pia, Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Jimbo la Mashariki Kaskazini, Geoffrey Massawe amewaomba wajumbe wa Bunge la Katiba kuungana na kuwa kitu kimoja katika mchakato wa kujadili Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba.
Kauli hizo za maaskofu hao zimekuja siku moja baada ya ile ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kusema kuwa hatima ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu utategemea Ukawa, kurejea katika Bunge Maalumu kuipitisha Katiba Mpya kwa wakati.
Askofu Massawe alitoa ombi hilo wakati wa ibada maalumu ya sherehe ya maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini iliyofanyika katika Kanisa la TAG Kinondoni, Dar es Salaam.
Akitoa salamu za TEC wakati wa kuadhimisha miaka 25 ya uaskofu ya Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa kwenye Uwanja wa Kichangani, Iringa, Makamu Rais wa TEC, Mhashamu Severine Niwemugizi alisema ni vyema wajumbe hao wakarudi kwenye Bunge hilo linalotarajia kuanza Agosti 5, mwaka huu.
“Ninatumia neno kuwataka na siyo kuwaomba warejee bungeni mwezi ujao. Wasipofanya hivyo au kufanya mizengwe mingine na kutupatia Katiba isiyotufaa, nitawaomba Watanzania wote tuweke uzalendo mbele na kuikataa Rasimu ya Katiba itakayoletwa pia tuwanyime uongozi katika Uchaguzi Mkuu ujao,” alisema.
Alisema wameshuhudia mambo ya aibu katika Bunge la Katiba kabla ya kupisha Bunge la Bajeti na maoni ya wananchi yaliyokusanywa kupitia tume halali yakibezwa.
Alisema tume ile iliongozwa na wazee wenye uzoefu mkubwa waliolitumikia taifa kwa muda mrefu na kutumia fedha nyingi za walipa kodi lakini yalipuuzwa jambo ambalo siyo sahihi.
“Nchi imepoteza dira, wananchi wako njiapanda hawajui kama watapata Katiba au la na ubinafsi umechukua nafasi kuliko uzalendo kwa taifa,” alisema.
Niwemugizi aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kuboresha Daftari la Wapigakura na kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na ule mkuu utakaofanyika mwakani.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu, Pinda aliwataka viongozi wa dini kuliombea taifa kuwa na amani kutokana na matukio makubwa ya Uchaguzi Mkuu na Katiba yaliyopo.
Pinda alisema amesikia ujumbe uliotolewa na Askofu Niwemugizi na kuwa kiongozi makini ni yule anayekubali kukosolewa na kufanya marekebisho.
Boti isiyotumia nahodha yavumbuliwa nchini
Mvumbuzi wa boti isiyotumia nahodha, Emmanuel Bukuku akitoa ufafanuzi wakati wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha naglory kundi
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi a Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini hapa jana, Mvumbuzi wa mashine hiyo, Immanuel Bukuku alisema kuwa imemchukua miezi sita kufanikisha uundaji wa mashine hiyo.
Alisema uvumbuzi huo umeambatana na majaribio ambayo yamefanyika katika Pwani ya Kigamboni na yameonyesha mafanikio makubwa na ipo tayari kwa ajili ya matumizi ikiwa na kamera za kutosha kwa ajili ya uchunguzi na kupeleka taarifa.
“Uvumbuzi umekamilika na boti ipo tayari kwa ajili ya matumizi na wadau wanakaribishwa kwa ajili ya kusaidia ufanikishaji wa utengenezaji wa boti nyingine zaidi,” alisema na kuongeza kuwa boti hiyo itakuwa inaongozwa na mashine nyingine itakayo kuwa sehemu maalumu.
Bukuku ambaye ni mwalimu wa masuala ya Sayansi na Teknolojia katika Chuo cha Veta Chang’ombe alisema amevumbua boti hiyo ambayo imetengenezwa kwa kutumia vifaa rafiki na mazingira ya bahari na inatumia mfumo wa umeme jua na mashine za kuzalisha umeme.
“Ina uwezo wa kuhisi kuwapo kwa mtu au chombo kingine jirani yake na kutoa taarifa katika sehemu ambako kinaratibiwa, pia ina uwezo wa kushambulia kwa kutumia mitutu na ina uwezo mkubwa katika masuala ya ulinzi na usalama,” alisema.
Alisema pia amefanikiwa kutengeneza injini ya ndege ambayo imeonyesha mafanikio kwa kiasi kikubwa na wakati wowote inaweza kutumika na mafanikio hayo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mpango wa Veta wa kuwa na Kitengo cha Masuala ya Ufundi na Ubunifu.
“Kuna mashine na teknolojia nyingi ambazo zimevumbuliwa hapa, ni dalili njema na tuna matumaini kuwa uvumbuzi zaidi unafuata kutokana na tafiti nyingi kuonyesha dalili za mafanikio,” alisema na kuongeza kuwa kitengo hicho kimepania kubadili mwelekeo mzima wa Veta kwa hivi sasa.na glory kundi










